TASAF KIGAMBONI WATOA MAFUNZO KWA KAMATI YA USIMAMIZI YA JAMII ILI KUWAJENGEA UWEZO KATIKA MAJUKUMU YAO
Leo 29/9/2022 Mratibu wa TASAF bi.Edda John Gweba kwa kushirikiana na Afisa Maendeleo ya jamii wa kata ya Mjimwema bi.Adnesta Josephat wametoa mafunzo kwa Kamati ya Usimamizi ya jamii ili kuwajengea uwezo katika majukumu yao.
Akizungumza Afisa Maendeleo ya jamii ambae pia ni Mwezeshaji wa Mpango wa TASAF wakati akitoa mafunzo hayo ameeleza malengo ya TASAF kwa undani ili wapate kujua kwa undani hasa na waweze kutekeleza majukumu yao wakizingatia malengo ya TASAF.
Mwezeshaji huyo wa Mpango wa TASAF alibainisha majukumu mbalimbali ya kila kiongozi katika kamati kama vile mwenyekiti,Muelimishaji,Mweka hazina na mlipaji namba moja.
Pamoja na majukumu ya kila kiongozi katika kamati mwezeshaji alifafanua majukumu ya kamati ambapo alisema kamati ina majukumu ya kusinamia shughuli za kila siku za utekelezaji wa mradi kama vile maadili katika kutumia fedha za ruzuku,utizaji wa masharti,kusinamia utekelezaji wa miradi ya jamii(PWP),manunuzi,ufuatiliaji wa maendeleo ya vikundi,usimamizi wa kutekeleza miradi ya kuongeza kipato na kutoa taarifa kwa serikali ya kijiji kila mwezi inayohusu utekelezaji wa shughuli zao.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa