Mkuu Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo ameiagiza wakala wa barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Wilayani humo kusambaza vifusi vyote vya barabara vilivyorudikwa kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu hiyo iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
D.C Bulembo ametoa agizo hilo leo Februari 26.2024 katika kikao cha ushauri cha Wilaya DCC kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi yake kwa lengo la kupitia mapendekezo ya rasimu ya Mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Akizungumza wakati wa kikao hicho DC Bulembo ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi, Manispaa ya Kigamboni kwa kutenga fedha kiasi cha Tsh Mil 20 kwa kila Kata kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara zitakazo saidia kupunguza adha ya usafiri kwa Wananchi Wilayani humo.
Aidha DC huyo ameitaka Menejimenti ya Manispaa ya Kigamboni kuwekeza katika fukwe ya Bahari kwa kuanzisha Miradi mbalimbali itakayosaidia Manispaa kukuza Mapato kupitia uwekezaji huo
Akijibu swali la mjumbe Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu Erasto Kiwale amesema Serikali inatambua changaomoto ya barabara ya Kibada Mwasonga na ilishatenga bajeti kwaajili ya ujenzi wa barabara hiyo kinachosubiriwa ni utiaji saini wa Mikataba ili ujenzi uanze mara moja.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa