Waziri wa ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ameiagiza wakala wa Barabara Tanzania TANROAD kuipitia na kufanya marekebisho sehemu zote za Barabara zilizoathirika na mvua za El nino kutoka Kibada- Mwasonga hadi Kimbiji ili kupunguza kero ya usafiri kwa Wananchi kabla ya Mkandarasi anayetarijia kuanza ujenzi wa Barabara hiyo kwa kiwango cha lami hajaanza kazi.
Mhe. Bashungwa ameto agizo hilo leo Novemba 15.2023 katika ziara yake yenye lengo la kukagua Barabara zote zilizo athirika na mvua za El Nino pamoja na zile zilizopo katika hauta ya ujenzi.
Hata hivyo kaimu Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) Injinia. Dorothy Mtenga amesema hatua zote za ununuzi wa vifaa zimeshakamlika na ujenzi wa Barabara hiyo yenye urefu wa kilimita 41 kwa kiwango cha lami utaanza mara baada ya zoezi la utiaji Saini wa Mikataba kukamilika.
Aidha Injinia Dorothy amesema ujenzi wa Barabara hiyo utagharimu kiasi cha Tsh Bil 83.8 ikiwa ni fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na mkataba wake unatajarajia kuwa wa miezi 20 mpaka kukamilika.
Akiongea wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo amesema kukamilika kwa Barabara hiyo kwa kiwango cha Lami kutapunguza adha ya usafiri kwa Wananchi wa Kata nne za Manispaa ya Kigamboni ambazo hutegemea Barabara hiyo katika kuendesha shughuli zao la kila siku.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa