Wafanyakazi wa Taasisis ya Kuzuia na kupambana na rushwa ( PCCB) wa Wilaya za Temeke na Kigamboni leo wamewataembelea wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni (Vijibweni) ambapo walipata muda wa kuongea na watumishi wa hospitali hiyo pamoja na wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata huduma.
Kamanda wa PCCB wa Wilaya ya Kigambopni ndg Philip Joseph amesema ziara hiyo ni katika kuadhimisha siku ya kupambana na rushwa na utoaji wa haki duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 9 Desemba kila mwaka ambapo wao kama sehemu ya jamii wanashiriki kujumuika na jamii kwa ajili ya kutoa elimu dhidi ya mapambano dhidi ya rushwa lakini pia kutoa zawadi mbali mbali kwa wahitaji.
Wakiwa hosipitalini hapo walitembelea wodi za watoto, wazazi pamoja na wodi ya akina baba ambapo walitoa zawadi za vyakula na vifaa vya kufanyia usafi kwa wagonjwa.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Dr. Charles Mkombachepa aliwashuruku kwa zawadi pamoja na elimu waliyoitoa kwa watumishi na wananchi katika hospitali hiyo na kusema rushwa ni adui wa haki na kila mtu anatakiwa kupinga rushwa kwani kwa mazingira yao ya kazi wanawahudumia wananchi ambao wengi wao hawana uwezo hivyo wanafika hospitali kutafuta huduma na si kuombwa rushwa.
Kauli mbiu ya mwaka huu dhidi ya rushwani" Piga vita rushwa ,zingatia maadili,haki za binadamu na utawala bora kuelekea uchumi wa kati''
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa