Afisa Tarafa wa kata ya Pembamnazi Bi. Loyce Mwasaga ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) kuacha kufanya kazi kwa mazoea, huku akiyaasa kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu.
Afisa tarafa huyo ametoa agizo hilo Agosti 21. 2024 alipo mwakilisha mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo katika kikao kazi cha mashirika yasiyo ya kiserikali kilichofanyika katika ukumbi wa jengo la Ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya.
Aidha ameyasihi kushirikiana na wananchi ili kujenga jamii iliyobora na yenye kuzingatia tamaduni ya mtanzania
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi zisizo za Kiserikali Wilaya ya Kigamboni Bwn Suma Nyembo amesema baadhi ya mashirika hayana uelewa wa kutosha kuhusu namna Bora ya kujiendesha na ameuomba uongozi wa Manispaa ya Kigamboni kuendelea kutoa semina za kuwajengea uwezo ili kuhakikisha wanajiendesha vyema kwa mujibu wa Sheria.
Naye Afisa Maendeleo Manispaa ya Kigamboni Bi. Neema Msuya ameyaasa Mashirika hayo kufanya kazi kwa kushirikiana, kujenga umoja wenye uongozi madhubuti ili kuweza kusimamia maslahi ya pamoja na kuongezea ufanisi katika kukuza uchumi wa nchi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa