leo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imezindua Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa siku 16 iliyobeba kauli mbiu ya “kila uhai unathamani, tokomeza mauaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto” kwa kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Paul makonda kwa lengo la kuchukua hatua madhubuti kama kizazi kinachoamini na kuthamini usawa wa kijinsia katika maeneo yote hapa nchini.
Akizungumza wajati wa uzinduzi muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Abdalla Kizega( Mtendaji wa Kata) amesema kuwa, ukatili unaanza sehemu yoyote hivyo wanafunzi wawetayari kutoa taarifa mapema pindi wanapoona viashiria vya ukatili ili kudhibiti vitendo hivyo kwasababu jambo hilo linatekekeza kizazi chetu.
Afisa ustawi Bi.Recho Ikamba wakati akitoa taarifa fupi amesema kuwa manispaa ya kigamboni chini ya Maafisa Ustawi na Maendeleo ya jamii kwa kushirikiana na wadau wanaofanya kazi pamoja na Halmashauri wataendelea kuadhimisha kampeni hii kwa kutoa elimu ili kupunguza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
Ameongeza kuwa Manispaa ya Kigamboni kwa kushirikiana na wadau pia imeendelea kuimarisha ujenzi wa vituo vya kijamii vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ambapo mpaka sasa kituo kilichopo Mbutu kata ya Somangila kimekamilika na kimeanza kutumika.
Aidha madawati ya kijinsia na watoto yameanzishwa katika vituo vya polisi Kigamboni ambapo hadi sasa kituo kimoja na vituo vidogo vya polisi na maafisa polisi maalumu wamepatiwa mafunzo ya jinsi ya kushughulikia mashauri ya ukatili.
Elimu ya ukatili wa kijinsia imetolewa kwa Shule 15 za Msingi na 6 za Sekondari, vituo vya bodaboda,vituo vya daladala, wamiliki wa day care na makao ya watoto walio katika mazingira magumu.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni katika kampeni hii ya siku 16 za kupinga ukatili imepanga kutoa elimu kwenye Kata ambazo hazijafikiwa na kuhuisha kamati za kupinga ukatili kwa Mwanamke na mtoto (MTAKUWA).
Afisa maendeleo Bi.Suzan Swai amewashukuru wadau wanaoshirikiana na Manispaa ambao ni Salama foundation,Kigamboni community centre, SMAUJATA, Woman Empowering and Entrepreneurship Development organization(WEEDO), Women Action Towards Economic Development (WATED) na Dawati la jinsia na watoto Polisi Kigamboni na kuomba wadau wengine kujitokeza ili kufikia lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa