Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni inatarajia kujenga soko la Kisasa katika Kata ya Kibada mtaa wa Kiziza katika mwaka wa fedha 2018/19 litakalogarimu kiasi cha shilingi bilioni 14 hadi kukamilika kwake.
Mradi huu unaotarajiwa kutoa ajira kwa wananchi zaidi ya mia tano kwa wakati mmoja utakuwa na sehemu za kuuzia bidhaa toka shambani, sehemu za kuuza bidhaa zilizochambuliwa, migahawa, maduka ya kawaida,taasisi za kifedha kama Benki pamoja na maduka ya kuuza na kununua fedha.
Mkuu wa idara ya Uchumi na ufuatiliaji wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Renatus Mchau amesema tayari mradi huu umewasilishwa katika ngazi mbali mbali kuanzia Mkoa , TAMISEMI na Benki ya dunia kwa ajili ya upembuzi yakinifu ambapo katika hatua zote hizo umepata baraka na sasa kinachosubiriwa ni utekezaji wake.
Mradi huu utakuwa na manufaa ya kipekee kwaManispaa ya Kigamboni na wakazi wa Kigamboni na maeneo jirani kutokana na kukosekana kwa soko rasmi la aina yoyote katika eneo la Manispaa nzima ya Kigamboni.
RAMANI YA PICHA ZA SOKO LA KISASA LINALOTARAJIWA KUJENGWA KIBADA.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa