SOKO LA KIMKAKATI KIBADA MANISPAA YA KIGAMBONI LAWA KIVUTIO KWA MADIWANI KUTOKA MJINI MAGHARIBI B
Katika muendelezo wa kutembelea miradi ya Manispaa Madiwani kutoka Mjini Magharibi B wamejikuta wakivutiwa na soko la Kisasa la Kibada Mali ya Manispaa ya Kigamboni .
Soko hili jipya la Kibada ambalo linategemewa kuanza hivi karibuni linajumuisha sehemu mbalimbali ambapo lina upande wa vizimba,maduka,ofisi,parking
Soko lipo katika kata ya Kibada ambapo limegharimu kiasi cha shilingi bil.6 mpaka kukamilika kwake chanzo cha pesa ni kutoka serikalini kuu.
Soko hili linategemewa kuiongezea Manispaa mapato kwa mwaka kiasi cha shilingi mil.211 kwa mwaka.Soko lina ukubwa wa Mita za mraba 5100.Tunamshukuru Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa zalizotekeleza mradi huu utakaoongezea mapato halmashauri.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa