Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeadhimisha siku ya Vijana Duniani kwa kufanya usafi katika Zahanati ya Kigamboni na kasha kushiriki mazoezi ya viungo katika viwanja vya shule ya msingi mji mwema.
Maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu ‘’Ushiriki na Ushirikishwaji wa vijana katika kudumisha amani’’ mgeni rasmi alikuwa Katibu tawala wa Wilaya ya Kigamboni Bi.Rahel Muhando aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo.
Mgeni rasmi aliwaasa vijana kutoruhusu kutumiwa na watu wengine kwa maslahi yao ambayo yanaweza kuzima ndoto zao. ‘Vijana wenzangu,nyie ni hazina kubwa,msikubali watu wengine kuwatumia kwa malengo yao’’ alisema mgeni rasmi. Aliongeza kuwa wapo watu wengi wanawatumia vijana katika mambo mbali mbali lakini wanapofanikiwa wanawashau na kuwaacha vijana wakiteseka bila kujua cha kufany.
Kwa upande wake mratibu wa Vijana katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Bi. Veronica Kiluvia aliwataka vijana kuunda vikundi vya vijana ili waweze kupata mikopo inayotolewa na Manispaa ya Kigambaoni ambapo kila mwaka Halmashauri hutenga asilimia Kumi ya mapato yake kwa ajili ya Vijana na akina mama.
Siku ya vijana uadhimishwa kila mwaka tarehe 12/08 ambapo vijana kutoka maeneo mbalimbali ya kigamboni zaidi ya mia tano walijumuika kwa pamoja katika siku hiyo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa