Baraza la Madiwani la halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni limekubali kwa kauli moja kupitisha sheria Nane ndogo pamoja na kanuni zake mpya za halmashauri kama zilivyowasilishwa na Mkurugenzi wa halamshauri ndg Stephen Katemba.
Utungaji wa sheri hizo kutahitimisha matumizi ya sheria za awali ambazo baadhi ya sheria ziliazimwa kutoka manispaa ya Temeke kutokana na Kigamboni kugawanywa toka Manispaa hiyo.
Sheria zilizowasilishwa na Mkurugenzi ni;
1. Sheria ndogo za ushuru wa huduma(service levy)
2. Sheria ndogo za ada ushuru
3. Sheria ndogo za matangazo
4. Sheria ndogo ya Megesho
5. Sheria ndogo za uvuvi na rasilimali za bahari ya Hindi
6. Sheria ndogo za masoko na mgulio
7. Sheria ndogo za usafi na mazingira
8. Sheria ndogo ya Burudani na
9 . Kanuni za kudumu za halmashauri
Akiwasilisha sheria hizo, Mkurugenzi aliiomba baraza la madiwani kukubali kupitishwa kwa sheria hizo baada ya hatua za awali kupitishwa katika kila kata na mitaa yake, ambapo wananchi walishirikishwa katika kutoa maoni na hivyo hatua iliyokuwepo sasa ni kupitishwa katika baraza la madiwani na kisha kupelekwa kwa mkuu wa mkoa kwa hatua zaidi ili ifikapo July 1,2018 sheria hizo mpya ziwe tayari kutumika .
Baada ya sheria hizo kupitishwa , diwani wa kata ya Kimbiji Mh. Sanya Bunaya alielezwa masikitiko yake juu ya muingiliano uliopo kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na Wizara ya Ardhi ambapo mpaka sasa wizara hiyo bado inaendelea na zoezi la upimaji na umilikishaji wa ardhi katika manispaa ya Kigambani pamoja na kuwa Mamlaka iliyokuwa chini ya wizara hiyo KDA kuvunjwa na majukumu yake yote kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Kigamboni. Hoja hiyo iliungwa mkono na madiwani wote akiwemo diwani wa kata ya Kigamboni Mh. Dotto Misawa ambaye alienda mbali na kumuomba Rais Dr.John Pombe Magufuli kuingilia kati suala hilo kwani kuna dalili za kutoelewana kati ya Wizara ya Ardhi na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa