SHERIA KUCHUKUA MKONDO WAKE KWA AMBAO HAWATASHIRIKI USAFI
Leo Tarehe 28/01/2023 wilaya ya Kigamboni imefanya zoezi la usafi wa jumamosi ya mwisho wa mwezi ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Mh. Enerst Mafimbo Ndamo akiongozana na Katibu Tawala wa wilaya ya Kigamboni ndg. James Mkumbo, Kaimu Mkurugenzi ndugu Juvenalis B. Mauna pamoja na wananchi wa wilaya ya Kigamboni.
Akiongea mara baada ya zoezi hilo la usafi Mh. Mstahiki Meya Enerst Mafimbo Ndamo amewapongeza waliojitokeza na kuwataka wananchi kushiriki kwa kujitokeza kufanya usafi wa jumamosi ya mwisho wa mwezi kwani zoezi limekuwa la kusuasua kwa baadhi ya wananchi .
Akisisitiza juu ya kushughulikia suala hilo Mh.Ernest amesema "Sisi kama Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa mwaka huu tutatumia sheria ndogo ndogo za Halmashauri kwa watakaokaidi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwani usafi ni wajibu wa kila mwananchi, inafika wakati usafi tunafanya viongozi wananchi hawajitokezi ipasavyo,wito wangu wananchi mjitokeze kufanya usafi usafi ni wajibu wetu."
"SAFISHA PENDEZESHA KIGAMBONI"
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI KGMC
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa