Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imejipanga kuendelea kuwawezesha wawekezaji wa ndani ili kuchochea ongezeko la wawekezaji na ukuaji wa mitaji.
Mhe. Majaliwa ameyasema hayo Leo Disemba 14, 2024, katika ziara yake katika kiwanda cha uzalishaji dawa za binadamu Cure Afya kinachomilikiwa na kampuni ya AfriCab, Kimbiji - Kigamboni.
“Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano wawekezaji, kuthamini na kuvifanya kuwa endelevu viwanda vya ndani kwa kutumia mikakati mbalimbali, ili kuhakikisha uwekezaji unaofanywa na wazawa unakuwa na tija” amesema Mhe. Majaliwa.
Aidha, Mhe. Majaliwa ameelezea umuhimu wa kuwa na wawekezaji wa ndani weny viwanda vinavyoongeza uzalishaji wa ndani wa bidhaa muhimu kama vile dawa za binadamu.
“Kujenga kiwanda hiki ni mchango mkubwa sana kwa Serikali, uwepo wa viwanda vya dawa nchini unasaidia upatikanaji wa haraka wa dawa, kwa gharama nafuu tofauti na kuagiza nje na kwa ubora tunaoweza kuusimamia, niwahimize tuu mtanue uwanda wa uzalishaji wa dawa hizi ili mfikie mahitaji mengine” amesema Mhe. Kassim Majaliwa
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa