DC Msafiri amewataka wanufaika wa mikopo kuzingatia urejeshaji wa mikopo ili na wengine waweze kunufaika.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati alipokua akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 165,385,000.00 kwa vikundi 26 vya wanawake, vijana na watu wenyeulemavu ikiwa ni asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa kipindi cha Julai- Septemba inayolenga kuinua uchumi wa wananchi.
Mkuu wa Wilaya amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imedhamiria kuwainua kiuchumi wananchi wake ili kuendana hali ya uchumi wa kati.
Aidha ameongeza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni katika jitihada za kuendelea kuwainua wajasiliamali wa kigamboni imeandaa eneo maalumu ambalo watapewa wajasiliamali kwaajili ya kufanya biashara ambalo pia linatarajiwa kujengwa stendi kubwa ya daladala.
Manispaa ya Kigamboni tangu imeanza kutoa mikopo imekwisha toa mikopo yenye thamani ya shilingili Bilioni 1,697,600.00 kwa vikundi 486 vyenye jumla ya wanufaika 4680,ambapo jumla ya shilingi 493,092,140.00 zimerejeshwa.
Mkuu wa Wilaya na wanavikundi mbalimbali wakiwa wameshika hundi ya mikopo ambayo imetolewa kwao.
Mwakilishi wa kikundi cha wakinamama cha gonga gonga kwa niaba ya wanavikundi wote akipeana mkono wa shukurani na Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri.
Hundi
Mkuu wa Wilaya Mhe Sara Msafiri akizungumza na vikundi vinavyopewa Mikopo.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri akikata utepe kala ya kuwakabidhi vijana waendesha bodaboda.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa