Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi jengo la Ofisi za walimu Katika Shule ya Msingi VIJIBWENI Katika Wilaya ya kigamboni ambapo hapo awali walimu walikosa ofisi kwa ajili ya kufanya kazi yao kwa ufanisi.
Ofisi hiyo ya kisasa ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 200 ambapo ndani yake ina ukumbi mikutano, Ofisi ya mwalimu mkuu, Mwalimu mkuu msaidizi,ofisi ya walimu wote, Chumba cha kuhifadhi mitihani, stoo, sehemu ya mapokezi, chumba cha kubadilishia nguo, vyoo vya kisasa na bafu huku ikiwa imefungwa viyoyozi (AC) ili kuhakikisha walimu wanafanya kazi kwa uhuru.
Akizindua ofisi hizo amesema dhamira yake ya kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira bora ipo palepale kwakuwa anatambua thamani ya mwalimu ni kubwa kwenye jamii hivyo wanastahili kupewa heshima.
Aidha ameishukuru Kampuni ya CRJE East Afrika ya nchini China iliyoamua kumuunga mkono kwa kujenga ofisi mbili za walimu kwa lengo la kuwawezesha walimu kufanya kazi katika mazingira mazuri.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa