Mkuu wakoa wa Dar es Salaam Mhe.Amosi Makalla ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa kuendelea kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo na kuwataka kuendeleza mwenendo huo.
Mhe. Makalla ametoa pongezi hizi kwenye kikao cha Baraza maalumu la kupitia hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwenye ukumbi wa Manispaa na kusema kuwa Halmashauri imejitahidi kuwa na hoja chache kwa mwaka 2021 kwani nyingi zilizopo ni za kipindi cha nyuma ambapo kati ya hoja 43, hoja 20 zimejibiwa na 23 zilizobaki kuhakikisha zinafanyiwa kazi kama ilivyoelekezwa.
Ameongeza kwa kusema kuwa pamoja na hati safi uongozi unapaswa kujikita katika kudhibiti upotevu wa mapato, kutumia asilimia 70 kwenye miradi ya maendeleo, kutumia asilimia 10 ya makundi maalumu na kutambua kuwa mwaka wa fedha ujao Serikali imeongeza asilimia 15 ya ukusanyaji mapato.
"Hatupaswi kutegema Serikali Kuu katika kutekeleza miradi wakati Halmasuari inao uwezo wa kukusanya mapato, tuhakikishe tunakusanya na kudhibiti upotevu wa mapato" Alisema Mkuu wa Mkoa.
Aidha Mkuu wa Mkoa amegiza uongozi wa Manispaa kudhibiti biashara holela kwa wafanyabiashara kufanya kazi kwenye maeneo rasmi na kutunga sheria ndogo zinatazotumika kusimamia , kulipa fidia kwa wale wanaodai, kulinda maeneo kwa kuwekea mipaka, kudhibiti migogoro ya ardhi, kuondoa malalamiko kwa wananchi juu ya dhuluma ziazofanywa na kampuni zinazouza ardhi kwa kuhakikisha wanafuata taratibu ili kuweze kuwahudumia Wananchi.
Pia Mkuu wa Mkoa amezielekeza Taasisi zote zenye umiliki wa maeneo Kigamboni kuhakikisha wanasafisha maeneo yao na kuyawekea mipaka ili kuondoa mapori kwani Kigamboni ndilo eneo pekee Dar es Salaam lililobaki kwa kuendeleza ujenzi hivyo si vyema kuwa na mapori.
Kuhusu utekelezaji wa Anwani za makazi awamu ya Pili ya kuweka vibao kwenye Nyumba na Barabara Mkuu wa Mkoa ameipongeza Kigamboni kwa kuendeleza vyema na kuwataka kumaliza zoezi vizuri huku wakiendelea kuhamasisha wananchi juu ya Sensa.
Mkuu wa Mkoa alitumia fursa hiyo pia kuwakumbusha wananchi juu ya zoezi la usafi linalofanyika kila mwisho wa mwezi na kusema kuwa kila mmoja aone anajukumu la kusafisha eneo lake kuanzia ngazi ya Kaya hadi kwenye maeneo ya kazi na biashara.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangassa amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa pongezi, kupokea maelekezo na kusema kuwa atahakikisha yote yanafanyiwa kazi ambavyo ameelekeza kwa kulenga kuongeza tija kwa maendeo ya Kigamboni ili kuweza kufikia malengo ya Serikali.
Angel Mosha Kaimu Mkaguzi Mkazi akiwsilisha taarifa za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuipongeza Kigamboni kwa kupata hati safi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akiipongeza Manispaa ya Kigamboni na kutoa maelekezo ya kufanyiwa kazi wakati wa kikao cha baraza maalumu .
Kuanzia kushoto ni Mkuu wa Wilaya Mhe. Fatma Nyangassa, Mkuu wa Mkoa Mhe. Amosi Makalla na Naibu Meya Mhe. Stephano Waryoba wakifatilia uwasilishwaji wa taarifa .
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almas Nyangassa akipokea maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa.
Baadhi ya madiwani wakifatilia uwasilishaji wa taarifa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg.Erasto Kiwale akitolea ufafanuzi wa hoja zilizotolewa na Madiwani wakati wa upokeaji wa taarifa za hoja za Mkuguzi Mkuu wa Hesabu wa Serikali
Baadhi ya Wataalamu wa Manispaa ya Kigamboni wakifatilia uwasilishaji wa taarifa ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Fedha Genoveva Meshi akitoa taarifa fupi ya Hoja za Serikali.
Baadhi ya Madiwani wakifatilia uwasilishwaji wa taarifa ya Hesabu za Serikali kwenye mkutano wa Baraza maalumu.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa