Leo Mei 10 2024 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miundombinu ya barabara ya Kibada kwenda Mwasonga Katq ya Kisarawe ii pamoja na barabara ya Kijaka Mwasonga iliyopo Kata ya Kimbiji Wilaya ya Kigamboni.
Akijibu maswali ya Wananchi wakati wa ziara hiyo RC Chalamila amesema Serikali inatambua changamoto ya Barabara hiyo ambayo imekuwa kero kwa Wananchi na amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameridhia barabara hiyo iweze kujengewa kwa kiwango cha Lami.
Aidha katika ziara hiyo Mheshimiwa Chalamila amewataka Wananchi Wilayani humo kuacha tabia ya kujenga mabondeni hali inayosababisha kujaa kwa maji katika makazi hayo na kuziba mitaro ya maji katika barabara.
"Kuna baadhi ya Wananchi wamekuwa na tabia ya kujenga mabondeni na wakiona mvua inanyesha huamia maeneo mengine na mvua ilikata wanarudi natoa wito Dar es Salaam haina mafriko ila tabia yetu ya kutofuata ushauri unaotolewa na viongozi." Alisema RC Chalamila.
Mkuu wa Mkoa huyo alihitimisha ziara hiyo kwa kufanya mkutano wa hadhara katika mtaa wa Mwasonga na Kijaka ambapo alisisitiza na kutatua kero za Wananchi Wilayani humo
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa