*Na Minde Honorata
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ameviagiza vyombo vya dola kuchunguza uhalali wa sh. milioni 800 iliyolipwa kwa Julius Maganga na kampuni ya upimaji na uuzaji wa ardhi inayojulikana kamamakazi estate" ambayo inatuhumiwa kuhusika na mgogoro wa umiliki wa ardhi katika eneo lililopo mtaa wa muhimbili kata ya Pemba Mnazi
Mhe. Chalamila ametoa maagizo hayo leo Agosti 18, 2023 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa eneo lenye mgogoro wilayani Kigamboni
Sambamba na hilo, ameagiza pia uchunguzi kufanyika kubaini kiasi cha kodi kilicholipwa kwa Serikali dhidi ya mauziano hayo na nani alilipwa
“OCD mliangalie hili swala kwa undani ikiwa ni pamoja na kuchunguza uhalali wa sh. Mil. 800 zilizolipwa na kampuni ya Makazi Estate kwenda kwa Julius Maganga,"amesema Chalamila.
Katika maagizo yake hayo, amevitaka vyombo hivyo vya dola kutumia hadidu za rejea za taarifa za awali za kamati iliyowahi kuundwa kufuatilia changamoto hiyo ili kuweza kuzichunguza zaidi nyaraka za wale wote wanaotuhumiwa kuhusika na mgogoro huo.
Ameelekeza kuwa endapo kutatokea mtu ambaye atakataa kuhojiwa kwa lengo la kusaidia kukamilisha uchunguzi huo, basi apatiwe taarifa haraka iwezekanavyo ili aweze kumchukulia hatua stahiki.
Katika kudhibiti uwezekano wa kuibuka mgogoro mwingine, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa maelekezo kwa Kamishna wa ardhi Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Shukrani Kyando kuwa kuanzia sasa kusitolewe hati zozote zinazohusiana na eneo hilo.
“Kuanzia sasa ni marufuku kutoa hati zaidi ya hizo ambazo zimeshatolewa na zile ambazo utakuja kujiridhisha mwishoni kama zinatakiwa kufutwa au kubaki,” amesema.
RC Chalamila pia ametoa maagizo kwa kamishna wa ardhi kupeleleza mchoro wa eneo la ardhi lenye ekari 150 kama taarifa za upimaji wa eneo hilo zipo ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni au la na akamuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa Erasto Kiwale kuanza kufanya uhakiki wa kina kuhusu wamiliki wa maeneo yote yanayoonekana kuwa wazi.
Aidha, amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni @halima_bulembo kwa kuanzisha clinic ya Ardhi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa