Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli leo amezindua Ghala la kuhifadhia gesi lenye uwezo wa kuhifadhi tani 7650 za gesi linalomilikiwa na kampuni ya Taifa Gesi ambayo awali ilikuwa ikijulikana kwa jina la Mihan Gas eneo la Vijibweni Wilayani Kigamboni .
Akizungumza wakati wa uzinduzi Mhe. Rais amesema kuwa Sekta ya Gesi ni sekta nyeti na muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote duniani, ni muhimu katika kuboresha huduma za jamii ikiwemo afya za wananchi , matumizi ya nishati bora ni muhimu katika kutunza mazingira, kwa kutambua hili chama cha mapinduzi kupitia Ilani yake ya 2015 iliahidi kushirikiana na sekta binafsi hivyo anfarijika kuona utekelezaji wa ahadi hiyo unatekelezwa kwa kiwango kikubwa.
Ameongeza kuwa anapongeza wizara ya nishati kwa jitihada kubwa ya kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini, na kwamba hali inaridhisha tatizo la kukatika katika kwa umeme pamoja na kwamba lipo baadhi ya maeneo kidogo lakini limepungua sana na wananchi wengi wameunganishiwa na umeme ikiwemo vijijini.
“kadri ya miradi hii inavyoendelea miradi ya umeme na gesi nina uhakika bei zitashuka ili wawekezaji wengi waweze kupata faida katika miradi yao watakayowekeza”
Amepongeza sekta binasfi kwa kuitikia wito na kuungana na Serikali katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini, akisema kuwa Mhe waziri wa nishati amesema nchi yetu inakampuni 8 zenye leseni ambazo zinatumika kusambaza gesi majumbani na viwandani hivyo kusaidia kutunza mazingira yetu kwa kupunguza matumizi ya mkaa.
Aliongeza kuwa Miongoni mwa kampuni inayofanya biashara ya gesi Taifa Gas, imewekeza kiasi cha bilioni 150 ikihusisha ujenzi wa maghala na mitambo ya kuhifadhi gesi kwenye mikoa 20, mojawapo ya maghala ni hilo ambalo amelizindua leo lenye uwezo wa kuhifadhi gesi tani 7650 ambapo limeifanya Taifa Gesi kuwa kubwa nchini, Afrika mashariki na kusini mwa janga la sahara .
Aidha amesema kuwa Ghala hilo limeongeza uwezo wa kuhifadhi gesi nchini kutoka tani 8050 mwaka 2016 hadi kufikia tani 15600 hivi sasa hivyo kuwapongeza, na kwamba amefurahi kuona wamiliki wakampuni hiyo kuwa ni watanzania, ambao wameonesha kuwa watanzania wanaweza hasa wanapoamua ambapo wameweza kutengeneza ajira na kulipa kodi na tozo mbalimbali.
“Serikali itaendeela kushirikiana nanyi na kamapuni zote zinazojishughulisha na biashara hii ya gesi lengo letu ni kuona wananchi wetu wanapata nishati bora, salama na kwa gharama nafuu” Alisema Mhe. Rais
Aidha ametoa wito kwa wasambazaji wa gesi ya mitungi kuendelea kutanua huduma zao hadi maeneo ya vijijini itawasaidia kupanua soko lakini pia nchi kutunza mazingira sababu asilimia 60 wananchi wanaishi vijijini na wanatumia kuni na mkaa ambayo sio nzuri sana kwa afya.
Pia ameitaka Wizara ya nishati kuongeza kasi ya kusambaza nishati ya gesi asilia meneo yote ambayo tayari kuna miundombinu na kutoa wito kwa watanzania hususani wanaoishi Dar es salaam kuacha matumizi ya mkaa kuanza kutumia gesi, ambapo mbali na kutunza mazingira na kulinda afya ni nafuu sana ukilinganisha na gharama za mkaa.
Mhe. Rais ametoa wito kwa Wasambazaji wa gesi majumbani kujaribu kupunguza bei ili kuhamasisha wananchi wengi kutumia gesi na kuacha matumizi ya mikaa ambayo ni uharibifu wa mazingira.
Mwisho Mhe Rais amewapongeza viongozi wa Kigamboni kwa namna ambavyo wameendelea kuiboresha kigamboni kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusema kuwa Kigamboni inakuwa na itaendelea kuboreshwa kwenye miundo yote ya Barabara, afya,, maji na sekta nyinginezo kwani ni Wilaya pekee yenye mpango bora wa makazi kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taifa Gesi mhandisi Hamisi Ramadhani amesema kuwa Hadi sasa wamefanikiwa kuwekeza mitambo ya gesi kwenye mikoa 20 na uwekezaji huo umefanyika ndani ya mwaka 2016 na 2018, ambapo baada ya uwekezaji huo Aprili mwaka 2019 walibadili jina kutoka Mihani Gasi na kuwa Taifa Gesi ili kuipa kampuni yao jina lenye asili ya nchi Yao baada ya kuwa na wamiliki wote watanzania na Uwekezaji huo unaifanya kampuni kuwa kubwa zaid kwenye uwekezaji kwa idadi ya mitambo ya kisasa ya Gesi mashariki na Kusini mwa Afrika ukiwa umegharimu takribani Bilioni 150.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa