Kauli hiyo imetolewa leo na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Bi. Dalmia Mikaya (Katibu Tawala Manispaa ya Kigamboni) alipokuwa akikabidhi pikipiki 9 zenye thamani ya shilingi milioni 23.1 kwa Watendaji wa Kata 9 wa Manispaa ya Kigamboni ikiwa ni uwezeshwaji wa vitendea kazi vitakavyowawezesha kutimiza majukumu yao vyema.
Dalmia amempongeza Mkurugenzi na menejimenti yake kwa kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya la kuwawezesha watendaji wa Kata ili waweze kutekeleza vyema majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuwafikia wananchi pale wanapowahitaji.
“Nawaomba sasa mkafanye kazi ,vitendea kazi hivi mkavitumie kwa shughuli za Serikali na kuleta matokeo chanya kwa wananchi na viongozi “ Alisema Katibu Tawala.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe.Ernest Mafimbo amameshukuru Mkuu wa Wilaya kwa wazo lake jema na waheshimiwa Madiwa kwa kuweza kupitisha fedha zilizomuwezesha Mkurugenzi kuetekeleza wazo hilo.
“Baraza la madiwani linaamini shughuli za serikali zitatekelezwa kwa ufanisi na sisi kama Madiwani tupo tayari kusimamia na kuhakikisha pikipiki hizi zinatumika kama ilivyokusudiwa”. Alisema Mhe. Mafimbo.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Bw. Wenslaus Lindi (Mkuu wa Idara ya Utumishi) amesema kuwa ni furaha kwa Manispaa kutekelezaji agizo la Mkuu wa Wilaya la kuwawezesha Watendaji wote wa Kata vyombo vya usafiri ambavyo vitawasaidia kutekeleza majukumu yao ili shughuli kama za ufuatiliaji wa Miradi ya maendeleo,mapato, vibali vya ujenzi na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika maeneo yao ya utawala zinafanyika vizuri..
Afisa Mtendaji Kata ya Somangila Bw. Muna Msafiri , amemshukuru Mkurugenzi na Madiwani kwa kuwapatia vyombo vya usafiri vitakavyowasaidia kuweza kufikia maeneo yote kwa kuzingatia ukubwa wa kata ambapo kipindi cha mvua ilikuwa ni changamoto kufikiwa kwa urahisi.
Halmashuri ya Manispaa ya Kigamboni ina Kata9 na watendaji wote wa Kata wamepatiwa usafiri wa Pikipiki.
Pikipiki za Watendaji wa Kata.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Bw. Wensalaus Lindi akitoa taarifa ya ununuzi wa Pikipiki kwa Viongozi.
Mtendaji wa Kata ya Vijibweni akipokea namba za Pikipiki atazyoitumia kwa utendaji wa kazi kutoka kwa Katibu Tawala Wilaya Bi. Dalmia Mikaya.
Mtendaji wa Kata ya Kisarawe II akipokea namba za Pikipiki atazyoitumia kwa utendaji wa kazi kutoka kwa Katibu Tawala Wilaya Bi. Dalmia Mikaya.
Mtendaji wa Kata ya Kigamboni akipokea namba za Pikipiki atazyoitumia kwa utendaji wa kazi kutoka kwa Katibu Tawala Wilaya Bi. Dalmia Mikaya.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Ernest Mafimbo akizungumza kwa niaba ya Madiwani.
Mtendaji wa Kata ya Somangila Muna Msafiri akishukuru kwa kupewa usafiri kwa niaba ya Watendaji wa Kata.
Watendaji wa Kata wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa Pikipiki zao.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa