Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga ametoa muda wa miezi 3 kwa uongozi wa Manispaa ya Kigamboni kukamilisha ujenzi wa nyumba za watumishi wa Kigamboni zinazojenga eneo la Gezaulole Kata ya Somangila.
Mhandisi Nyamhanga ametoa agizo hilo leo katika ziara yake aliyoifanya kwa lengo la kukagua na kutembelea utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo alitembelea eneo la Gezaulole zinapojengwa nyumba 25 za watumishi wa Manispaa ya Kigamboni, Hospitali ya Wilaya pamoja na ujenzi wa Madarasa 4 shule ya Sekondari Aboud Jumbe.
Aidha katika ziara hiyo Mhandisi Nyamhanga kuitia wizara yake ameahidi kutoa fedha kiasi cha Tsh Mil 10 kwaajili ya kuweka Vigae katika Madarasa mapya 4 Shule ya Sekondari Aboud Jumbe na pia ameridhishwa na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na ameipongeza Manispaa kwa kuanza kutoa huduma ya Afya katika Hospitali hiyo
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga alipotembelea kwenye Hos[pitali ya Wilaya kuona maendeleo
Baadhi ya wakuu wa Idara wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa nyumba za watumishi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga akizungumza jambo alipokuwa kwenye Shule ya Sekondari Abdu Jumbe
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga akiwa ameambatana na viongozi mbalilmbali kutembelea na kuona miundombinu kwenye Shule ya Sekondari Abdu Jumbe
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa