“Nawakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza Kigamboni kwasababu tunanishati ya umeme wa kutosha wa kuweza kuhudumia viwanda na matumizi mengine ya kwaida”.
Hiyo ni kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri mara baada ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme cha Dege ambacho kimekamilika kwa kuweza kuzalisha umeme wa Megawatts 48 ambapo hadi sasa jumla ya megawati 24 ndio zinazotumika kwa matumizi ya viwandani na majumbani kwa Wilaya yote ya Kigamboni na kubakiwa na ziada ya Megawats 24.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara alisema kuwa Kigamboni ilikuwa na changamoto mbili ya umeme na barabara ambapo changamoto ya umeme imekwisha malizika kabisa kwani Tanesco wameweza kugawa vituo vinne vya kusambazia umeme vya Muongozo 33kv, Kimbiji (Viwanda) 33kv, Kisarawe II (Viwanda) 33kv na Pembamnazi 33kv.
Mhe. Sara aliendelea kwa kusema kuwa kwa sasa eneo pekee Dar es salaam linaloweza kuwekweza viwanda ni Kigamboni kwa sababu kwanza ni eneo la kimakakati ambalo hata master plan yake imeweza kuainisha maeneo ya uwekezaji lakini pia, Serikali ilikwisha tenga fedha ya miundombinu ya barabara ambayo kwa mwaka wa fedha ujao unaonza Julai barabara hizo zitakuwa zinaanza kujengwa kwa kiwanago cha lami ikiwemo ile ya Kibada-Kisarawe II hadi Kimbiji.
“Nawapongeza sana Tanesco kwa kazi kubwa waliyoifanya kwenye Wilaya yetu na Serikali kwa kutoa fedha nyingi kuhakikisha tunamaliza changamoto ya umeme,mradi umegharimu Bilion.26 huduma ya umeme imeboreshwa, wananchi wa Kigamboni fanyeni shughuli zenu kwa uhuru”DC Sara.
Aliongeza kuwa Tanesco wamesaidia kupata wawekezaji wakubwa kwani idadi ya maombi ya kuunganishiwa umeme imeongezeka kutoka 200 hadi 1000 na kuunganisha wateja wapya 800 kila mwezi kutoka wateja 500 hapo awali.
Niwatake Tanesco kutokana na mahitaji makubwa na shughuli za kiuchumi kuwa za uhakika, tunaomba mfanye Kigamboni kuwa Mkoa wa Kitanesco ili iweze kujitegemea kibajeti na kutengeneza mfumo wa kiutawala wa kuweza kuwahudumia wananchi kwa uhakika.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Bara za la wafanyabiashara Elicontro Mrema alisema kuwa anaishukuru Serikali kwa jitihada kubwa ya kuimarisha nishati ya umeme Kigamboni kwa kuondoa ule upungufu uliokuwa unatatiza wawekezaji kuja kuwekeza.
Mkuu wa Wilaya alifanikiwa kuwatembelea wawekezaji wakubwa wawili mmoja akijulikana kwa jina la ELSEWEDY watakaojihusisha na utengenezaji wa kebo na transfoma wanaojenga kiwanda chao eneo la Kisarawe II ambao wanatarajia kuanza uzalishaji mwanzoni mwa mwezi wa nane na kutarajia kuajiri watumishi 400-500 wa kitanzania’
Kiwanda cha pili ni AFRICAB-CURE AFYA PHARMACETICAL kinachojengwa Kimbiji watakaojihusiah na uzalishaji wa aina mbalimbali za dawa wanaotarajiwa kumaliza ujenzi wa kiwanda Desemba mwaka huu na kuanza uzalishaji Januari 2022 wakilenga kuajiri watumishi 200-400 wa kitanzania.
Kituo cha kuzalishia umeme cha Dege kikiwa kimekamilika na kuanza matumizi tangu 30/04/2021
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sara msafiri akielekezwa na Meneja wa Tanesco namna mifumo inavyofanya kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri akimutoa rai ya kuifanya Kigamboni kuwa ya Kimkoa Kitanesco ili iweze kujisimamia yenyewe kwa kuwa na rasilimali watu wa kutosha na vifaa vya kutosha.
Muwekezaji wa Kiwanda cha ELSEWEDY akimueleza Mkuu wa Wilaya namna kiwanda chake kilivyolenga kuwaaajiri na kuwafundisha watanzania hususani wale wanafunzi waliotoka kuhitimu masomo yao ili waweze kuwa waalimu kwa wenzao.
Muwekezaji wa Kiwanda cha ELSEWEDY akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni uwekezaji wanaoufanya na namna walivyojipanga kumaliza kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri akiwa amemambatana na wataalamu kutoka AFRICAB na Wenyeviti wa Baraza la Biashara Kigamboni wakizunguka kuangalia uwekezaji wa kiwanda hicho cha kutengeneza dawa.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri akizungumza na Meneja Masoko wa AFRICAB juu ya uwekezaji na kiwango cha watumishi atakaowaajiri.
Kiwanda cha ELSEWEDY kinachotarajiwa kuzalisha kebo , transfoma na magenereta na kulenga kuhudumia wateja wa Africa Mashariki na nje .
Kiwanda cha Africab cure pharmaceutical kinachotarajiwa kuzalisha dawa mbailmbali za binadamu na kuhudumia wateja wa Africa mashariki, Afrika ya Kati na Kusini.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa