Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Halima Bulembo ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kutekeleza shughuli zao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu bila kuathiri tamaduni za jamii ya Tanzania.
Hayo ameyasema leo wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa Mashiriki ya kiserikali ( NGO),Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigamboni.
Mh. Bulembo aliongeza kwa kusema yapo mashirika yanafanya vizuri katika kuisaidia jamii ila yapo baadhi ambayo yamekua chachu ya kuleta mmomonyoko wa maadili unaopelekea kuleta sintofahamu ndani ya jamii.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji Mkurugenzi Mtendaji wa Eden Garden foundation shirika linalosaidia wadada wanaojiuza bi. Martha Minja amesema mpaka kufikia mwezi Mei,2023 tayari wamefanikiwa kutoa elimu kwa walengwa 58 hasa wale wanaojiuza katika maeneo mbali mbali ndani ya Manispaa ya Kigamboni.
Bi. Minja aliendelea kwa kusema jumla ya walengwa 58 tayari wameshapatiwa huduma ya ushauri wa namna ya kukabiliana na kuachana kabisa na biashara ya kuuza mwili kwa kushirikiana na idara ya ustawi wa jamii.
Wilaya ya Kigamboni kupitia ofisi ya Mkurugenzi Manispaa imefanikiwa kusajili jumla ya mashirika 41 yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi na Halmashauri ya Wilaya.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa