Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto ambaye pia ni mbunge wa Kigamboni Mh.Dr Faustine Ndugulile, alionesha kufurahishwa na mafanikio yaliyofikiwa na akina mama wa Manispaa ya Kigamboni katika maonesho ya siku tatu katika viwanja vya Mji mwema Kigamboni.
Maonesho hayo yaliyowajumuisha akina mama toka katika kata tisa za Manispaa ya Kigamboni yalianza leo tarehe 25 na kuhitimishwa siku ya jumamosi ya tarehe 27/01/2018.
Katika siku ya kwanza ya maonesho hayo, Naibu Waziri alifika akiwa ndiye mgeni rasmi, alipata nafasi ya kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na akina mama hao. "Nimepita kila banda, nimeona bidhaa zenu, mnajitahidi sana nami nawaahidi kuwaunganisha na taasisi zetu kama TFDA,SIDO na TBS ili bidhaa zenu ziweze kutambulika kitaifa na kimataifa" alisema Ndugulile.
Aliongeza kuwa bidhaa za akina mama zina uhusiano wa moja kwa moja na jamii zetu hivyo ni lazima sisi kama jamii na viongozi tuwaunge mkono ili waweze kufikia malengo yao ya kuwa na viwanda vidogo vidogo ndani ya manispaa na taifa kwa ujumla.
Naye Mratibu wa jukwaa la akina mama Bi.Edda Gweba , aalisema wana vikundi vya akina mama zaidi ya 80 ndani ya manispaa ambavyo vinavyozalisha bidhaa mbali mbali , hivyo wao kama halmashauri wanajitahidi kuwapa elimu ili waweze kuzalisha bidhaa bora zinazozingatia mahitaji halisi ya walaji na afya kwa ujumla. Ameongeza kuwa changamoto inayowakabili ni soko la uhakika la bidhaa zao kwani endapo watapata soko la uhakika watazalisha bidhaa bora zaidi na pia kuwawezesha kupiga hatua ya maendeleo.
Maonesho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu "wanawake tumia Jukwaa la wanawake Kufikia uchumi wa Viwanda'' yalihitimishwa siku ya jumamosi ya tare 27/01 /2018 katika viwanja vya shule ya Msingi Mji Mwema ambapo wageni na watu mbali mbali walifika katika viwanja hivyo kujifunza teknolojia mbali mbali na pia kujipatia bidhaa zinazozalishwa na akina mama katika vikundi na viwanda vidogo vidogo ndani ya manispaa ya Kigamboni.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa