Naibu waziri wa Afya,Wazee jinsia na watoto na Mbunge wa Manispaa ya Kigamboni Mhe.Faustine Ndugulile amekabidhi vitanda na magodoro 14 vinavyotarajiwa kuhudumia wagonjwa wa dharula kwenye Hospitali ya Vijibweni na kuwataka wataalamu kuvitumia vitanda hivyo kwa lengo lililokusudiwa.
Mhe.Ndugulile ameyasema hayo leo alipokuwa akikabidhi vitanda alivyopokea kutoka kwa jamii ya Australia (Australia Tanzania society) na kampuni ya JACANA ikiwa ni matokeo ya mkakati ambayo Serikali inashirikisha sekta binafsi katika hali ya utoaji wa huduma za Afya.
Amemtaka Mkurugenzi wa Manispa ya Kigamboni na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni kusimamia mapato na kuhakikisha mifumo ya kudhibiti mapato inafungwa kwenye vituo vyotevya afya ili fedha zitakazopatikana zitumike kuboresha huduma nyingine za afya.
Aidha Mhe.Ndugulile amesisitiza ofisi ya Mkurugenzi kuweka mfumo mzuri wa malalamiko ili kuwarahisishia wananchi wanaokuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma kujua waende kwa nani kuweza kuhudumiwa na kusikilizwa malalamiko yao.
“ Mkurugenzi Mtendaji,Mganga Mkuu wa Wilaya na Mganga Mfawidhi wekeni tangazo la namba za simu kwenye bango i ili mwananchi akiwa na malalamiko ajue anampigia simu nani, tunataka uwazi na uwajibkaji kwenye serikali ya awamu ya tano”. Amesema Mhe.Ndugulile
Pia Naibu Waziri amesema ni vizuri Wilaya na hospitali kujipanga na kuhakikisha dawa zote za msingi zinakuwepo kwa mujibu wa muongozo, Serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka Biloni 30 hadi Bilioni 66, bajeti ya dawa imeongezeka mara hivyo inahitaji dawa hizo ziwanufaishe wananchi , sambamba na hilo ameagiza duka la dawa lifunguliwe na kutoa miezi sita kukamilisha zoezi hilo.
Naibu Waziri pia amewapongeza watumishi wa Hospitali ya Vijibweni na kuwataka kufanya kazi kwa kujitoa na kuwahudumia wananchi kwa lugha nzuri mbali na uchache wa watumishi walionao,huku akihitaji idadi ya watumishi wanaohitajika.
“Rushwa , matusi nisingependa kusikia na sitakubali kutolea tarifa za ubora wa huduma sehemu nyingine lakini kwangu hakupo vizuri, Mkurugenzi na Mganga Mkuu simamia hilo, mtu yeyote atakayebainika hatutashindwa kumshughulikia”Amesema Mh.Ngugulile
Afisa uhusiano wa JACANA Bw.Ahmed Merere amesema sera zao ni kujali jamii kila mahali wanapofanya kazi ,wanataka kuona jamii zinakuwa bora na mikakati yao ni kuchangia katika masuala ya afya, elimu , maendeleo ya jamii hususani miradi ya kinamama na Vijana, hivyo ni faraja kwao kukabidhi vitanda hivyo.
Hospitali ya Vijibweni imeanzishwa mwaka 20016 na inahudumia wagonjwa 430 kwa siku sawa na wagonjwa 154,800 kwa mwaka.
kutoka kushoto ni Naibu waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Mh.Faustine Ndugulile ,Bw.James Chialo Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, Afisa Uhusiano wa JACANA Bw.Ahmed Merere, Meya wa Manispaa Mh.Hoja Maabad wakipokea vitanda
Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Mh.Faustine Ndugulile wa kwanza kushoto akipeana mkono wa shukurani na Afisa Uhusiano wa JACANA wakati wa Makabidhiano ya vitanda.
Naibu Waziri wa Afya akiwasisitiza watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili.
Naibu Waziri wa Afya akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh. Hoja Maabad akiwashukuru wafadhili kwa msaada wa vitanda
Afisa uhusiano Bw.Ahmed Merere kutoka JACANA akizungumzia lengo la kusaidia Hospitali ya Vijibweni .
Baadhi ya Vitanda vya kuhudumia wagonjwa wa dharula vilivyokabidhiwa Hospitali ya Vijibweni leo na Naibu Waziri wa Afya.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa