Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Kigamboni kujenga majengo ya Kituo cha Afya Kigamboni kwa kufuata ramani ya sasa inayotumika kwenye vituo vyote Tanzania nzima.
Maelekezo hayo ameyatoa leo alipotembelea kituo hicho cha afya na kubaini kuwa jengo la upasuaji halijaungana na jengo la mama na mtoto na kumtaka Mkuu wa Wilaya kusimamia ujenzi wa majengo hayo kwa kuhakikisha yanaungana kama muongozo unavyoelekeza.
“ Ramani inayotumika ilikuwa bado haijafanyiwa maboresho nimeelekeza majengo yajengwe kwa kuzingatia ramani ya sasa yaani jengo moja linakuwa na chumba cha upasuaji na jengo la mama na mtoto,ni matarajio yetu kwamba mama anapojifungua iwe kwa njia ya kawaida au kwa upasuaji tukikutana naye tukute ana mtoto ili kupunguza adha kwa mama hususani katika kipindi hiki ambacho huduma za mama na mtoto zinasogezwa karibu” Alisema Naibu Waziri.
Akizungumzia eneo la soko katika kata ya Kibada, Naibu Waziri amesema kuwa eneo lipo vizuri na ukubwa unatosheleza, zaidi ni kuhakikisha wanafatilia maandiko ili ujenzi wa soko uanze mara moja, kwasababu linatarajia kuwa chanzo cha uhakika cha mapato kwa Halmashuari na kuondoa adha kwa wananchi kwa kwenda umbali mrefu kufata huduma na wafanyabiashara kupeleka bidhaa zao .
Aliongeza kuwa eneo la stendi liongezwe kama wataalamu walivyoeleza kwa kufikia mita za mrada 16000 ambalo litakidhi haja na kuwa stendi ya uhakika lakini pia chanzo cha mapato cha uhakika kwa Halmasuri husika.
Kwa upande wa ujenzi wa jengo la Halmashauri amesema kuwa ujenzi unaendelea vizuri lakini hajapata taarifa nzuri ya kasi ya ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwasababu ya kuchelewa kupata majibu ya sampuli ya kupima udongo lakini wamekubaliana kuwa kasi ya kuchimba msingi itaongezeka.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri amesema kuwa maelekzo yote yaliyotolewa na Naibu waziri atakaa na wasaidizi wake kwa kushirikiana na Mkurugenzi na kwamba marekebisho ya haraka yatafanyika kwenye kituo cha Afya ili kukidhi vigezo vya ramani iliyotolewa kwasababu ujenzi bado upo kwenye hatua za awali.
Naibu Waziri amefanya ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Wilaya ya Kigamboni ambayo italeta tija kwaajili ya kusaidia wananchi, ambapo alitembelea eneo linalotarajiwa kujengwa soko na stendi lililopo Kata ya Kibada, ujenzi wa jengo la Utawala linalojengwa Somangila na upanuzi wa kituo cha afya cha Kigamboni.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni (kulia) Arch.Ngw'ilabuzu Ludigija akimpokea Naibu Waziri TAMISEMI Mhe.Josephat Kandege alipowasili kwenye ofisi za Wilaya ya Kigamboni.
Naibu waziri Tamisemi Mhe. Josephat Kandege akizungumza na viongozi na baadhi ya watumishi mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wilaya ya Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri akitoa utangulizi kwa Naibu Waziri TAMISEMI alipofika kwenye ofisi yake Kabla ya kuanza ziara yake .
Mchumi Ruperto M. Mboya (Mratibu wa uwekezaji) akielezea mpango wa ujenzi wa soko na stendi ya mabasi itakayojengwa Kata ya Kibada.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ngw'ilabuzu Ludigija akitoa maelezo ya ujenzi wa soko la kisasa Kata ya Kibada.
Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege na Mkurugenzi wa Manispaa Arch.Ngw'ilabuzu Ludigija wakitazama ramani ya ujenzi wa soko la kisasa litakalojengwa Kata Kibada.
Mhandisi wa Manispaa Bw.Pius Mtechura akitoa maelekezo ya mpangilio wa majengo katika ramani kwa Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege.
Ukaguzi wa ujenzi jengo la utala ukiendelea
Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege mwenye suti ya kijivu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa jengo la utawala.
Naibu waziri TAMISEMI akiwa ameambata na viongozi mbalimbali wakitoka kuangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo la utawala Somangila.
Naibu waziri TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege wa kwanza kushoto akitazama eneo la ujenzi wa jengo la mama na mtoto
Eneo linalojengwa jengo la mama na mtoto na mafundi wakiendeleana kazi.
ukaguzi wa eneo la ujenzi wa jengo la upasuaji .
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa