Kamati ya siasa Mkoa ya Chama cha Mapinduzi ikiongozwa na Mwenyekiti Wa Mkoa Bi.Kate Kamba na katibu Wa chama Mkoa Bw. Zakharia mwansasu Leo wamefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Manispaa ya Kigamboni ikiwa ni utekelezaji Wa Ilani ya chama.
Mwenyekiti Wa Mkoa na katibu wamefurahishwa na maendeleo ya Ujenzi Wa majengo ya ofisi ya Mkuu Wa Wilaya na Mkurugenzi yanayojengwa Somangila, Ujenzi Wa Hospitali ya Wilaya na shule ya sekondari Kigamboni na kusema kuwa malengo ya ukamilishwaji Wa majengo hayo yafanyike kwa wakati uliopangwa ili wananchi waweze kupata huduma kwa karibu.
Aidha uongozi Wa chama umepongeza Manispaa kwa kutekeleza Miradi ( mradi wa shule ya sekondari kigamboni) kwa kutumia Mapato yao ya ndani mbali na uchanga walionao.
Wakizungumzia upande Wa barabara ambazo zipo chini ya Tarura , wamesema kuwa Kigamboni bado haina miundombinu mizuri ya Barabara na bajeti inayopangwa ya Bilioni 2.1 kwa mwaka kwa utekelezaji ni ndogo ambayo haiwezi kufikia mahitaji , na kusema ni vyema ikapangwa mikakati ya kuhakikisha miundombinu ya barabara inaboreshwa.
Aidha Mkurugenzi Wa Manispaa ya Kigamboni Ameshukuru uongozi Wa chama Wa mkoa kwa ziara waliyoifanya na kusema kuwa maelekezo yote waliyoyatoa yatafanyiwa Kazi kwani yeye pamoja na wataalamu wake wamehipanga kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati na wananchi wanapata huduma wanayoitarajia kutoka kwa Serikali inayowaongoza.
Miradi iliyotembelewa Leo ni Ujenzi Wa Majengo ya Ofisi ya Mkuu Wa Wilaya na Mkurugenzi, Ujenzi Wa Hospitali ya Wilaya, Ujenzi shule ya sekondari ya Kigamboni na barabara ya Maweni-Tungi-Vijibweni.
Mwenyekiti wa chama Mkoa wa kwanza mbele Bi. Kate Kamba akiwa ametoka na wataalamu kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
ukaguzi wa jengo la kuhifadhia dawa
ukaguzi jengo la utawala la hospitali
Muonekanao wa ndani wa jengo la utawala
Mafundi wakiendelea na taratibu za kuweka miundombinu ya umeme kabla ya kupiga lipu
ukaguzi wa barabara ya maweni-tungi-vijibweni
Barabara ya Maweni-Tungi-Vijibweni
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa