Na. Minde Honorata
*Meya Kigamboni aelekeza usimamizi fedha za miradi*
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Ernest Mafimbo amewataka Madiwani kusimamia matumizi ya fedha zilizowekwa kwenye akaunti za kata zikiwa na lengo la kutekeleza ujenzi na maboresho ya Miundo ya barabara.
Meya Mafimbo ameyasema hayo leo Agosti 15, 2023 kwenye kikao cha baraza la madiwani kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kigamboni.
Meya Mafimbo ambaye ni Diwani wa Kata ya Tungi amesema zipo fedha zilizotengwa kulingana na miongozo inayoelekeza kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kila mwaka na kuzielekeza kwenye ujenzi wa barabara na tayari wameziwasilisha kwa lengo la maboresho ya kazi hizo hizo.
"Sisi tunajivunia mazingira ya utekelezaji wa hili agizo tuna fedha ambazo tunazo kwenye akaunti za kata na zile zilizoenda TARURA kabla ya muongozo huu mpya," amesema Meya Mafimbo.
Amesema kuwa fedha zilizotolewa zina maelekezo maalum na pindi watakapoanza kuzitumia wahakikishe wanafata sheria, kanuni na taratibu zote za manunuzi huku wakifuata miongozo kutoka kwa wasimamizi wa ujenzi wa bara bara (TARURA) ili kuepuka hoja zisizo za lazima.
"Tukasimamie hizo fedha wakati wa utekelezaji kusiwe na ujanja ujanja wa matumizi ya fedha hizo," ameonya Meya huyo.
Naye meneja wa TARURA Manispaa ya Kigamboni Bw.John Chacha amesema ujenzi wa barabara zilizoainishwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 utaanza ifikapo Septemba mwaka huu na kwa sasa hatua za ununuzi kwa wakandarasi zipo kwenye Makubalia
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa