Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Bi. Happy Luteganya leo amewahakikishia ushirikiano mkubwa shirika la lisilo la kiserikali la Building inclusive society lenye lengo la kuhakikisha vijana wenye ulemavu wa Kigamboni wanapata elimu sahihi kuhusu afya ya uzazi salama pamoja na haki na wajibu wao.
Mkuu wa Maendeleo ya jamii amebainisha hayo alipokua akifungua utambulisho wa mradi huo kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Wilaya unaojulikana kwa jina la “Uchechemuzi wa haki ya afya salama ya uzazi kwa vijana wenye ulemavu”
Happy alisema kuwa kwa niaba ya viongozi wake , mradi wao umepokelewa na Kigamboni ipo tayari kushirikiana nao ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala wa Shirika hilo Bw. Wanjara Sulusi amesema kuwa wanashukuru kwa ukarimu na muitikio waliouonesha wanakigamboni katika kupokea mradi na kwamba, wanatarajia watakapokuja kwa utekelezaji watapata ushirikiano mkubwa ili kufanikisha lengo la kujenga jamii jumuishi isiyombagua mtu kutokana na ulemavu alionao.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria ufunguzi was mradi.
Hilda Kifanga Afisa ustawi wa jamii akitoa mapendekezo ya kuboresha utekelezaji wa mradi
.
Washiriki waliohudhuria ufunguzi wa Mradi
Mkurugenzi wa utawala kwenye shirika Wanjara Sulusi akishukuru kwa mapokezi.
Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Happy Luteganya akizungumza wakati wa ufunguzi.
Viongozi wakifatilia maoni ya kuboresha mradi
Mratibu wa mradi Mussa Joseph akielezea mradi unavyolenga kufanya kazi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa