Hongereni Wilaya ya Kigambon kwa kutekeleza vizuri zoezi la Anuani za makazi kwa awamu ya kwanza na ya pili, sehemu iliyobaki naomba mtekeleze vizuri zaidi’
Ni kauli ya waziri wa habari na mawasiliano Mhe.Nape Nnauye wakati alipokua akitoa maelekezo matatu ya kufanyiwa kazi baada ya kupokea utekelezaji wa zoezi la anuani la makazi wilaya ya kigamboni kwenye ukumbi wa mkuu wa wilaya ya kigamboni wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa zoezi.
Waziri Nape amesema kuwa Kigamboni imetekeleza vizuri sana katika zoezi hili na kuwaomba kuendelea kufanya vizuri zaidi katika zoezi lililobaki la kuweka vibao vya namba kwenye kila nyumba na nguzo za barabara .
Wazri Nape ameongeza kwa kusema kuwa baadhI ya maeneo ambayo yanamigogoro ya umiliki kama maeneo ya jeshi, uwekezaji, hospitAli na mengineyo ,anauni za makazi hazitawekwa hadi migogoro hiyo itakapopatiwa ufumbuzi kwani kwa kuweka anuani wakati kunamigogoro ni kuhalalisha umiliki kinyume cha taratibu.
Aidha amesema kuwa viongozi wahakikishe majina ya mitaa yanaamuliwa na wananchi sambamba na kuhakikisha majina yanayotumika yaweze kutunza historia ya eneo husika na viongozi kutakiwa kuhakikisha wanashawishi wananchi kuridhia majina yanayoonekana kutunza historia ya maeneo yao.
Waziri amewataka viongozi kuanzia ngazi ya Wilaya hadi wajumbe wa nyumba kumi kuhakikisha wanahamasisha wananchi kushirki kwenye zoezi hili la anuan za makakazi kwani kuna nyakati zitafika mwananchi hataweza kupata huduma mbalimbali kama asipokuwa na anuani inayomtambulisha.
Naye Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. David Silinde ametumia fursa hiyo kuzitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakamilisha zoezi la anunani za makazi kabla ya kufikia mei 30 kwani hakuna sababu itakayopelekea Halmashauri yoyote kushindwa kufikia malengo kwaua miongozo ya utekelezaji yote imekwishatolewa ikiwemo ya kutumia fedha za mapato ya ndani.
‘Niweke wazi Halmashauri itakayoshindwa kufikia malengo hatutasita kuichukulia hatua za kinidhamu”Alisema Naibu Waziri.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amosi Makalla meshukru ujio wa Waziri na Naibu Waziri na kusema kuwa kwa ngazi ya Mkoa zoezi limetekeleza kwa namna yake na wapo tayari kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almasi Nyangassa ameshukuru kwa ziara ya kikazi ya viongozi iliyolenga kukagua utekelezaji wa zoezi na kuahidi kuyafanyia kazi malelekezo yote yaliyotolewa ili kufikia lengo la Serikali lililowekwa.
Ikumbukwe Kigamboni ilikadiria kuzifikia anuani za nyumba 49,353 anunani zilizoingizwa kwenye mfumo ni 58,508 sawa na 118.5%, Makadirio ya barabara yalikuwa 1,864 na zilizoingizwa kwenye mfumo 3,617, idadi ya barabara zilizowekwa nguzo ni 85 ambapo 26 zimewekwa katika zoezi hili na 59 ziliwekwa na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) mwaka 2018. Jumla ya namba za majengo ya makazi na Ofisi za Serikali 47 zimewekwa.Aidha Wilaya ya Kigamboni ilishika nafasi ya kwanza katika zoezi la Ukusanyaji wa taarifa za Anuani na Makazi.
Waziri wa Habari Mhe. Nape NNauye akikagua uwekwaji wavibao vya namba na anuani kwenye ofisi za Serikali ya Mtaa wa Feri .
Viongozi akiwa kwenye Mtaa wa Feri kukagua utekelezaji wa zoezi la uwekaji vibao vya barabara.
Waziri wa Habari na Mawasiliano Mhe. Nape NNauye akiipongeza Kigamboni na kutoa rai ya kumaliza vizuri utekelezaji wa sehemu iliyobaki.
Baadhi ya Viongozi na watumishi waliofika ofisi za Mkuu wa Wilaya Kigamboni kumpokea na kumsikiliza Waziri wa Habari na Mawasiliano Mhe.Nape Nnauye.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe.David Silinde akitoa maelekezo ya utekelezaji wa zoezi la anuani za makazi nchi nzima.
Diwani wa Kata ya Kigamboni Mhe. Dotto Msawa akiwaelezea viongozi namna anavyotekeleza zoezi la anuani za makazi kwenye Kata yake.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumzia mkoa namna ulivyofanikisha zoezi na Kuipongeza Kigamboni kwa kuongoza kimkoa kwenye utekelezaji wa Anuani za Makazi.
Mkuu wa Wialaya ya Kigamboni akikaribisha viongozi na kupoea malekezo ya uboreshaji wa utekelezaji wa Anuani za makazi kwa sehemu iliyobakia.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa