Hayo yamejiri Leo katika viwanja vya Mjimwema katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa afya bure ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Almas Nyangasa alikuwa Mgeni Rasmi.
Akiongea katika zoezi hilo litakalochukua siku mbili mfululizo Leo jumanne 7 Juni na jumatano 8 Juni Mhe.Nyangasa amewataka wananchi wa Kigamboni kujenga tabia ya kucheki afya zao mara Kwa mara ili kujitambua mapema iwapo wana maradhi katika miili yao ili kujitibia mapema kabla tatizo halijawa kubwa kwani ,Matatizo ya kiafya ni makubwa na changamoto hii imekua kutokana na kutofatilia afya zetu mara Kwa mara Kwa kuzichunguza ili kutatua tatizo mapema.
Pamoja na hayo Mheshimiwa DC ametoa tahadhari katika kuendelea kujikinga na tatizo la Uvico 19 na kuwasihi kuendelee kuchukua tahadhari ikiwepo kupata chanjo ambayo inapatikana pia katika zoezi hilo, aidha amewataka kuendelea kuwataarifu na wengine kufika kupata huduma.
Aidha amemshukuru mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kupatikana Kwa huduma hizi kupitia maagizo yake Kwa watendaji wake wa chini na uhusiano mzuri na wadau.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amepata nafasi ya kutembelea mabanda yote ya Wadau waliokuwapo hapo( likiwepo Banda la Kigamboni Manispaa ambapo wanatoa elimu ya lishe Kwa ajili ya kulinda afya na kuepukana na magonjwa) wakitoa huduma bure na kupata maelezo ya kina kuhusu huduma zinazotolewa .Amewashukuru wadau wote waliojitokeza kufanikisha zoezi hili na kuwataka kuendelee kuwa na moyo wa kujitolea.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Lucas David Ngamtwa,amewashukuru wadau waliojitokeza kutoa huduma bure,aidha amewasisitizia wananchi waendelee kufika kwani zoezi linaendelea ambapo kutakuwa na madaktari mbalimbali bingwa kutoka muhimbili watakaotoa huduma za uchunguzi wa afya.
Nae Naibu Meya wa Manispaa ya kigamboni Mhe.Stephano Warioba Kwa niaba ya Mstahiki Meya amewashukuru watoa huduma ya kucheki afya,amewataka wananchi kuzingatia ushauri watakaoupata ili kuepuka kupata matatizo zaidi ,amewataka wananchi kufika kwa wingi kupima afya zao ,na kuwataarifu na wenzao kuhusu zoezi hili ili waje kwa wingi kuangalia afya zao.
Wadau mbalimbali wameshiriki kutoa huduma ya upimaji afya bure wakiwepo Management for Health Development ( MHD) ambao wametoa sapoti kubwa kuwezesha zoezi hilo lakini pia wametoa huduma ya utoaji chanjo ya Uvico 19, akiongea Mratibu wa chanjo Kwa wilaya ya Kigamboni ndg.Martha Nkya wao amesema wako bega Kwa bega katika kuunga mkono juhudi za serikali katika masuala ya afya ili kujenga taifa lenye watu wenye afya na kuleta maendeleo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa