Leo Februari ari 20. 2024 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo amefanya ziara ya kuwatembelea Wavuvi katika Kata ya Pembamnazi pamoja na Kimbiji kwa lengo la kuongea nao na kusikiliza changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao za kila siku.
Akizungumza na wavuvi hao katika ziara hiyo DC Bulembo amepiga marufuku Uvuvi haramu unaofanywa na baadhi ya wavuvi ambao hutumia uvuvi huo kujinufaisha wenyewe huku wakiharibu mazalia ya samaki pamoja na viumbe wengine wanaoishi baharini
Hata hiyo Mheshimiwa D.C amewataka Wavuvi wote ndani ya Wilaya ya Kigamboni kuhakikisha wanakukata leseni za Uvuvi ili kurasimisha shughuli zao na amewataka kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali.
"Hatutamfumbia macho mvuvi yoyote anayefanya uvuvi haramu na Serikal itaendelea kuwachukuli hatua wale wote wanaojishughulisha na uvuvi huo." Alisema DC huyo.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi, Manispaa ya Kigamboni Ndugu Aron Bullu amesema idara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama WWF wamekuwa wakitoa elimu juu ya mbinu mbalimbali za uvuvi ili kuimarisha sekta hiyo ambayo inamchango mkubwa katika uchumi wa nchi.
Pia ameeleza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikitoa mikopo ya Boti kwa vikundi mbalimbali ambapo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Manispaa ilipotokea Boti 1 yenye thamani ya Tsh Mil 86.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa