Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Sara Msafiri leo kwa niaba ya Mkuu wa Moa wa Dar Es Salaam Mhe.Paul Makonda amewapokea Vijana waendesha baiskeli (EACBIKE TOUR) kutoka nchi tano zinazounda jumuiya ya Afrika Mashariki wenye lengo la kuhamasisha mtangamano imara kwa wananchi .
Akizungumza nao leo walipofika ofisini kwake Mkuu wa Wilaya amesema kuwa , Mkuu wa Mkoa amepata majukumu mengine ya kikazi hivyo amemuagiza kuwapa ujumbe wa kuwapongeza kwa uzalendo wao walio nao na kwamba waendelee kudumisha umoja na mshikamano katika nchi zetu ili upendo na amani viendelee kutawala katika Jumuiya yao.
Aidha mkuu wa Wilaya ameakaribisha vijana hao tena hata mara baada ya kumaliza mbio zao za kuhamasisha mshikamano kwa wananchi wapatapo nafasi kufika kwenye Ofisi zake na za Mkuu wa Mkoa kusalimia nao watafurahi kuwaona tena Vijana wao.
“ Tumefurahi hamkujali changamoto za foleni za Mji wa Dar es Salaam na maeneo yake, lakini mmefanikiwa kutembea maeneo mengi, tunawashukuru na umoja huu udumu “ Alisema Mkuu wa Wilaya.
Vijana hao waendesha baiskeli kutoka Nchi tanao zinazoundaJumuiya ya Afrika Mashariki wameshukuru na kusema kuwa wamependa mapokezi mazuri waliyoyapata na wameyapokea yote waliyoelekezwa.
Safari hizi za baiskeli wameanzia Kampala kupitia Kenya-Tanazania-Burundi-Rwanda na Baadae kumalizia tena kwa kurudi Uganda.
Kijana Muendesha Baiskeli akitoa umshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni kwa mapokezi na maelekezo waliyopewa.
picha ya pamoja na mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri aliyevalia vazi la kitenge.
kijana kutoka Tanzania akipita na baada ya pendera ya umoja wa nchi za Afrika Mashariki kupeperushwa kuashiria safari imeanza
Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri akiwakaribisha vijana waendesha baiskeli kutembelea ofisini kwake na kwa Mkuu wa Mkoa pindi wapatapo nafasi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa