“Niwatoe hofu chanjo ni salama, hapa nilipo ninawiki mbili tangu nichanjwe naendelea na shughuli zangu nawashauri kutumia nafasi hii kupata chanjo hususani makundi ainishwa”
Ni kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangassa leo alipokuwa akizindua zoezi la utoaji chanjo lililofanyika kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni iliyopo Gezaulole na kusema kuwa chanjo ni hiari lakini ni jambo la muhimu hasa kwa kuangalia nchi zilizotutangulia kupata chanjo namna ambavyo wameweza kupata matokea chanya ya kupunguza vifo.
Mkuu wa Wilaya amesema Kuwa chanjo iliyoletwa ni 1500 lakini mpaka sasa siku ya tatu chanjo tayari ni pungufu ya 1000 hivyo, ni lazima wananchi kuelewa kuwa hili ni jambo muhimu hasa kwa makundi ambayo yamepewa kipaumbele.
“Jukumu la afya ni la mtu binafsi, sisi kama Binadamu tunafanya kadri Mungu anavyotujalia ili kulinda afya zetu, ni lazima tuelewa madhira mengine ya chanjo ni matokeo ambayo yanaweza kutokea hata kwa chanjo nyingine kwasababu binadamu tumetofautiana” alisema Fatma
Aidha Mkuu wa Wilaya amatoa rai kwa wataalamu wa Afya na waliokwisha pata chanjo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya uelewa wa umuhimu wa chanjo, faida zake na mahali zinapopatikana ili kusaidia chanjo kuwafikia wananchi wengi kwani lengo ni kuhakikisha watanzania wanakuwa salama.
Ameongeza kwa kusema kuwa wananchi wote hata ambao wamekwisha kupata chanjo wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari zinazoelekezwa ili kuendela kujikinga na maabukizi ya UVIKO 19
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kigamboni Henry Chaula amesema kuwa ni vyema wananchi wakafuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu badala ya kusikiliza maneno yamitandaoni na kusema kuwa wao kama viongozi wanaunga mkono msimamo wa Serikali kuhusu umuhimu wa wananchi kupatiwa chanjo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Dkt.Ikaji Rashid amesema kuwa Manispaa imepokea Jumla ya dozi 1500 kwa kuanzia ambazo zimepelekwa kwenye maeneo ya kutolea chanjo ya Hospitali ya Wilaya Kigamboni dozi 500, Hospitali ya Vijibweni Dozi 500, Zahanati ya Kibada dozi 300 na kituo cha afya Kimbiji Dozi 200 na dozi nyingine zitaletwa kadri ya mahitaji.
Ameongeza kuwa chanjo inatolewa kwa watumishi wa afya,watu wenye umri zaidi ya 50 na wenye magonjwa sugu ambapo tangu chanjo imeanza kutolewa kwa siku mbili jumla ya wahudumu wa afya na wananchi 509 wamepatiwa chanjo kwa hiari yao .
Uzinduzi ulihudhuriwa na viongozi wa Chama cha mapinduzi ngazi ya Wilaya, Madiwani, viongozi wa dini, wananchi na wataalamu wa Wilaya ya Kigamboni.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Dkt.Ikaji Rashid akimuelezea Mkuu wa Wilaya na viongozi wengine namna utaratibu wa kupata chanjo unavyofanyika tangu mteja anavyopokelewa.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Almasi Nyangassa akikata utepe sanduku lililohifadhiwa chanjo ishara ya uzinduzi rasmi wa utoaji chanjo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Almasi Nyangassa akifungua sanduku lenye chanjo mara baada ya kukata utepe wa ufunguzi ili kujiridhisha na uwepo wa chanjo hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Almasi Nyangassa akishirikiana na muhudumu wa afya kunyanyua sanduku la chanjo ishara ya kufuhia uzinduzi rasmi wa chanjo ya Uviko 19
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Bw. Henry Chaula akipokea chanjo mara baada ya uzinduzi
Mwananchi Christoms Malingumu akipokea chanjo mara baada ya ufunguzi
Mkuu wa Idara ya Kilimo na Umwagiliaji Priscilla Mhina akipokea chanjo mara baada ya uzinduzi.
Katibu wa CCM Wilaya Bw. Evarist Mluge akipatiwa chanjo mara baada ya ufunguzi.
Diwani wa Kata ya Mjimwema Mhe.Omary Ngurangwa akipata chanjo mara baada ya uzinduzi.
Diwani viti maalumu Elizabeth Kimambo akipata chanjo mara baada ya uzinduzi.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipango miji na Maliasili Said Swalehe akipata chanjo mara baada ya ufunguzi.
Naibu Meya na Diwani wa Kata ya Somangila Mhe. Stephano Waryoba akipata chanjo wakati wa uzinduzi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa