MKUU WA WILAYA YA KIGAMBONI AWATAKA MAKARANI WA SENSA WATAKAOPITA KATIKA USAILI KUWA WAZALENDO WAKATI WA UTEKELEZAJI WA ZOEZI LA KUHESABU WATU NA MAKAZI
Hayo yamejiri Leo 19/7/2022 wakati wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Fatma Alma's Nyangasa ambae pia ni Mwenyeketi wa Kamati ya Sensa Wilaya ya Kigamboni alipotembelea katika kata ya Tungi na Kigamboni ili kujionea jinsi zoezi la usaili wa Makarani wa Sensa na wasimamizi wa maudhui Sensa,linavyoendelea na kujua iwapo kuna changamoto zozote ili zipatiwe ufumbuzi.
Akiongea akiwa katika ofisi ya kata ya Kigamboni Mkuu wa Wilaya amewaasa wasailiwa hao na kuwataka watakapita katika usaili huo kuwa waadilifu,waaminifu na kufanya kazi kwa uzalendo ili kuleta tija katika zoezi hili muhimu kwa taifa ambalo nibmsingi muhimu katika kupanga mapingo mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa Tanzania.
"Uhakika wa idadi kamili itakayopatikana baada ya zoezi hili la Sensa utapelekea serikali kupanga mipango yake ya maendeleo kwa wananchi na kujua mahitaji halisi Kwa wananchi wake ,ikiwepo idadi za shule kulingana na idadi ya vijana waliopo eneo husika,mbali na Hilo idadi ya zahanati na mengine mengi"alisema Mh.Fatma Alma's Nyangasa.
Kwa Wilaya ya kigamboni zoezi la usaili limeanza Leo na litaendelea kwa siku ya Kesho tena 20/7/2022 na matangazo yenye orodha ya majina ya waombaji walioitwa kwenye usaili yamebandikwa katika ofisi za kata hivyo waombaji wanatakiwa wafike katika kata zao kuangalia majina yao.
Sensa ya watu na makazi inatarajiwa kufanyika tarehe 23/8/2022 .
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI MANISPAA YA KIGAMBONI
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa