Kufuatia ukusanyaji mdogo wa mapato ndani ya Manispaa ya Kigamboni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri amelishauri baraza la madiwani na wataalamu wa Manispaa kujikita kwenye kubaini vyanzo vipya vya mapato ili kuwezesha manispaa kutekeleza shughuli za maendeleo kwa kiwango kinachotakiwa husuani katika kipindi hiki ambacho Serikali imejikita katika ukusanyaji wa mapato.
Mhe. Sara amesema hayo leo alipokuwa kwenye kikao cha Baraza maalum la kupokea taarifa ya fedha ya mwaka 2017/2018 lililofanyika kwenye ukumbi wa Kisota na kueleza kuwa kuwa, Manispaa ikiwa na mapato shughuli za maendeleo zitakwama au kutekelezwa katika kiwango cha chini kutokana na fedha kutotosheleza.
“Naomba tushirikiane Manispaa yetu haipo vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato, Mkuu wa wilaya , Waheshimiwa madiwani na wataalamu tushirikiane ikiwezekana tuunde timu ambayo itasimamia mambo ya uwekezaji pekee hata kwa kushirikiana na wadau kutoka nje ya Manispaa ambao ni wataalamu wa mambo ya uwekezaji” Alisema Mhe. Sara
Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe.Amin Mzuri Sambo alisema kuwa sasa imefika wakati Manispaa kuvuka viwango vya ukusanyaji mapato kwasababu maeneo ya uwekezaji yapo ya kutosha na mengine yanahitaji uendelezwaji tu hivyo ni kazi ya wataalamu kuandaa mipango mikakati itakayotekelezwa ili kuiwezesha Manispaa isonge mbele.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw. Charles Lawiso alisema kuwa yeye pamoja na wataalamu wapo tayari kuhakikisha wanapanga mipango mikakati inayotekelezeka ili mapato yaweze kuongezeka na kuisaidia Manispaa kujiendesha hususani shughuli za maendeleo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa