Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri amewaahidi wananchi wa Kata ya Kigamboni kushirikiana na wataalamu ili kushughulikia mifereji inayoziba kipindi cha mvua na kusababisha maji kujaa kwenye maeneo ya makazi na tassisi za umma na kuwataka wananchi kushiriki nguvu kazi pindi itakapohitajika.
Kauli hiyo ameitoa jana alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi iliyolenga kujitambulisha na kutambua changamoto zinazowakabili wakazi wa Kigamboni ili kuona ni naman gani zinaweza kushughulikiwa kwa kushirikiana na wananchi na wataalamu wa Manispaa.
Mkuu wa Wilaya alisema kuwa Kigamboni ni uso wa Wilaya nzima hivyo inapaswa kuwa kivutio kwa watu wanaoingia Kigamboni ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara kutoka kwenye barabara za vumbi kuwa za lami kila mtaa.
Aidha aliwataka wanawake vijana na watu wenye ulemavu kujikwamua na umaskini kwa kutumia vyema fursa ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali kwa kujiunga kwenye vikundi vya biashara ili waweze kupata mikopo na kuinua hali zao za kiuchumi.
"Vijana acheni kuwategema wazazi na kubeti, hamuwezi kujikwamua kwa kucheza biko na kubeti, kujikwamua kwenye umasikini ni kuamua kutoka kwenye nafsi zenu,amueni kwa kujiunga kwenye vikundi muweze kupata mikopo"Alisema Mhe.Sara
Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya aliwataka watumishi waliopo ngazi ya Mtaa kuwahudumia wananchi kutatua kero wanazokabiliana nazo badala ya kutegemea viongozi wa juu wakati kero nyingine zinaweza kutatuliwa na viongozi waliopo kwenye mitaa na kata.
Aliongeza kuwa tatizo linaposhindikana kwa ngazi mtaa na kata ndio ielekezwe kwa uongozi wa juu lakini isitokee wananchi kuzungumiza kero zao pindi viongozi wakubwa kama mkuu wa mkoa na mawaziri wakati Wilaya yenyewe inauwezo wa kutatua kero zao.
Mkuu wa Wilaya amemaliza ziara ya kutembelea Kata zote tisa za Wilaya ya Kigamboni kwa kujitambulisha na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
|
||
Viongozi wakiwa kwenye msafara kuelekea viwanja vya Swala Tuamoyo Kigamboni kwenye mkutano wa hadhara . |
|
Katibu Tawala Wialaya ya Kigamboni Bi.Rahel Mhando akitambulisha viongozi waliofika kwenye mkutano huo wa hadhara. |
|
|
|
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Hoja Maabad akisalimia wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara. |
|
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya alipokuwa akizungumza nao. |
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa