Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Amos Makala amewataka wataalamu wa idara ya Ardhi Manispaa ya Kigamboni kuhakikisha wanatatua kero za wananchi kwa juhudi zote ili kuepuka migogoro.
Mheshimiwa Makala ametoa wito huo mchana wa leo katika Mkutano wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika katika uwanja wa Mjimwema ikiwa ni utaratibu aliyouanzisha kwa lengo la kuwafikia wananchi katika majimbo yao.
"Niwahakikishie katika utaratibu huu nitakuwa nanyi kusikiliza hadi hatua ya mwisho nimejitoa kuwatumikia ntakuwa nanyi hadi hatua ya mwisho." Alisisitiza
Aidha kwa upande mwingine amesema kuwa ameuanzisha utaratibu huu kwa majimbo ya pembezoni kwa lengo la kumfikia kila Mwananchi.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mheshimiwa Ernest Ndamo Mafimbo amempongeaza mkuu wa mkoa kwa utaratibu mzuri aliyouanzisha kwa kuhamishia shughili zake Majimboni kwa kusikiliza kero za wananchi na ameomba utaratibu huu uendelee.
Pia Mheshimiwa Mafimbo ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuchanja chanjo ya ugonjwa wa corona ikiwa ni njia sahihi ya kujilinda na ugonjwa huo.
Sambamba na hilo mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Fatma Almasi Nyangassa ameeleza kuwa Wananchi wa Kigamboni wamefarijika sana kwa ujio wa Mkuu wa mkoa na wako tayari kuwasilisha kero zao
Ziara ya mkuu wa mkoa itazunguka mkoa mzima kwa lengo la kuwafikia wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa