“Sisi kama Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam tunaahidi kuandaa mazingira mazuri ya uwekezaji ili wawekezaji wapate fursa ya kuwekeza.”
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Amos Makala alipotembelea kiwanda cha kuzalisha vifaa vya umeme ikiwemo Transifoma Nyaya za umeme za ndani na nje ya nyumba cha Elsewedy kilichopo kata ya Kisarawe ii Manispaa ya Kigamboni.
Mheshimiwa Makala ameupongeza uongozo wa kiwanda hicho kwa kuwekeza katika Mkoa wa Dar es Salaam kwani uwepo wake utasaidia kupunguza gharama ya kuagiza vifaa toka nje ya nchi
Aidha katika ziara hiyo Mheshimiwa Makala ametoa wito kwa wawekezaji kuwekeza katika sekta ya nishati kwani fursa zipo nyingi hususani katika kipindi hiki ambapo Serikali inatekeleza sera ya kuhakikisha kila Kijiji kinapata nishati ya Umeme.
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Makala pia alitembelea mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Mpira Pamoja na Mabweni yanayojengwa na shirikisho la soka Tanzania (T.F.F) ambapo ametoa wito kwa Shirikisho hilo kuanzisha shule za kukuza kipaji cha mpira wa miguu kwa vijana wadogo ili kuongeza chachu katika mchezo wa Soka.
Mheshimiwa Makala akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Elsewedy
Mheshimiwa Makala akionyeshwa shughuli za ujenzi zinazoendelea katika kiwanda cha Elsewedy
Mheshimiwa Makala akisalimiana na Diwani wa Kata ya Kisarawe ii
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa