Februari 20, 2025 – Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Ndg. Erasto N. Kiwale, leo amewasilisha mapendekezo ya Rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 katika kikao cha Baraza la Madiwani.
Kwa mujibu wa rasimu hiyo, halmashauri inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi 61,374,426,952.34 kutoka vyanzo mbalimbali. Kati ya fedha hizo, shilingi 20 bilioni zinatarajiwa kutoka mapato ya ndani, shilingi 29.35 bilioni kwa ajili ya mishahara, na shilingi 1.65 bilioni ni ruzuku ya matumizi ya kawaida kutoka Serikali Kuu. Aidha, shilingi 5.56 bilioni zimetengwa kwa miradi ya maendeleo kupitia ruzuku ya Serikali, huku shilingi 4.8 bilioni zikitoka kwa wahisani na wafadhili.
Mkurugenzi Kiwale alitumia nafasi hiyo kuwashukuru madiwani kwa ushirikiano wao katika mchakato wa kuandaa rasimu hiyo, pamoja na wataalamu wa halmashauri waliotoa mchango wao wa kitaalamu kuhakikisha mpango huo unakidhi mahitaji ya maendeleo ya Kigamboni.
Aidha, amesisitiza kuwa bajeti hiyo imelenga kuboresha utoaji wa huduma za kijamii, kuimarisha miundombinu, na kusukuma mbele miradi ya maendeleo katika manispaa. Baraza la Madiwani linatarajiwa kujadili na kuidhinisha mpango huo kwa utekelezaji katika mwaka wa fedha ujao
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa