Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng’wilabuzu Ludigija leo amepokea msaada wa madawati 150 na bando 14 za mabati zenye thamani ya Milioni 20 kutoka Benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya benki ya kurejesha faida kwa jamii.
Akipokea msaada huo kwenye shule ya Msingi Mjimwema Mkurugenzi amesema kuwa ,Wilaya ya Kigamboni ni mpya bado ina mahitaji ya miundo mbinu ikiwa ni pamoja na madawati sababu kumekua na idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga darasa la kwanza na kidato cha kwanza,hivyo ni imani yake kunapokua na wadau kama NMB wanaounga mkono Serikali inafarijika kwani hawataki kuona mtoto anakaa chini sababu ufundishaji unakua mgumu.
Mkurugenzi amesema kuwa NMB wamekua na ushirikiano mzuri na wamekuwa wakisaidia Manispaa katika huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitanda vya kujifungulia na oparasheni walivyotoa hivi karibuni kwenye kituo cha Afya Kigamboni .
“NMB wamekua karibu kila mwaka wanatusaidia na sio mara moja hivyo tunashukuru pia kwa msaada huu wa madawati, Nashukuru na naahidi nitaendelea kushirikiana nanyi katika kuhakikisha kigamboni inakua na maendeleo”Amesema Mkurugenzi
Ameongeza kuwa Kutokana na mchango mkubwa unaoupata Manispaa kutoka NMB, Manispaa inataka washirikiane nao kwa kiasi kikubwa ndio maana kutokana na changamoto mbalimbali inayokabiliana nazo imeamua kufungua akaunti ambayo itawezesha kukusanyia mapato ya ndani lakini pia asilimia 10 inayoenda kuwezesha makundi maalumu ya vijana wanawake na walemvu itakua ikipitia NMB na mikopo itakapokuwa inatolewa itatokea huko.
Mkurugenzi amewashukuru pia walimu kwa jitihada wanazofanya za kutoa elimu kwa wanafunzi mbali na changamoto wanazokabiliana nazo na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa weredi kwani anatambua na kuthamini mchango wao katika ukuaji wa Elimu.
Mkuu wa Mahusiano Serikalini (NMB) Bi. Vicky Bishobu amesema anashukuru na kupongeza jitihada ambazo zinafanywa katika kukuza elimu,pia kuona NMB ni mahali ambapo Manispaa imeweza kwenda kuomba ushirikiano ili waweze kuwa sehemu ya jitihada nzuri katika kukuza sekta ya elimu”
Bi.Vicky Bishobu amesema kuwa Benki inakabidhi madawati 150 yenye thamani ya milioni 15 kwenye Shule za Msingi za Ufukoni ,Kibugumo na Amani gomvi na mabati bando 14 yenye thamani ya Milioni 5 na kusema kuwa wanaamini kuwa dawati 1 wanaka wanafunzi 5 haitakua imemaliza tatizo lakini imepunguza kwa kiasi jitihada za kuhakikisha wanafunzi wanakua na mazingira mazuri ya kusoma .
Aidha amesema kuwa kwa niaba ya Benki anamshukuru Mkurugenzi kwamba tangia amekuja amewaunga mkono na amekuwa mwepesi katika kujibu maombi yao ya kutaka kushirikiana zaidi na serikali hasa kusaidia katika jitihada za kukusanya mapato kwenye Halmashauri na Vituo vya Afya ambapo hatua iliyofikiwa ni nzuri na wameridhika nayo.
“ ni kitu ambacho hatukua nacho, kwa niaba ya Benki naomba uendelee kutuamini na utupe nafasi ili tuweze kushirikiana na kuhakikisha kwamba mianya yote ya kupotea kwa mapato inazibwa na sisi tunakua sehemu ya jitihada nzuri ya kuboresha mapato ili kuhakikisha huduma za kijamii zinakua nzuri”. Amesema Vicky
Tunashukuru pia kwa kuitikia wito wa kuchangamkia fursa katika benki tunaendelea kuhakikisha huduma zetu zinabioreshwa zaidi ili kuona ni sehemu ya kupata huduma nzuri, msisite kutushirikisha maeneo mengine ambayo Benki inaweza ikafanyia kazi.
Akisoma taarifa ya miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari kwa niaba ya Afisa elimu Wilaya Frank Makingi (Afisa elimu Vifaa na takwimu) Amesema kuwa Hali ya miundombinu katika shule bado haikidhi mahitaji kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo shuleni hivyo wadau mablimbali wa ndani na nje ya Halmashauri wanaendelea kualikwa kuunga mkono katika kuboresha miumbombinu ya madawati, vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo ili mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji shuleni yawe bora.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa