Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Bw.Ng'wilabuzu Ndatwa Lubigija ametoa shukrani kwa uongozi wa NMB Kigamboni pamoja na NMB Makao Mkuu kwa msaada wao wa Vitanda katika kituo cha Afya cha Kigamboni kata ya Kigamboni.
Akipokea Msaada huo, Mkurugenzi amewashukuru Banki ya NMB kwa msaada huo ambao ni muhimu kwa wananchi wake wa Kigamboni kwa ujumla kutokana na kituo hicho kuwa sehemu inayofikika kirahisi kuliko vituo vingine ndani ya Manispaa. Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni tano unahusisha vitanda tisa vya kujifungulia na vya kulaza wajawazito umetolewa na Banki ya NMB Tawi la Kigamboni kwa kushirikiana na makao makuu.
Akikabidhi msaada huo, Meneja wa Kanda ya Dar es salaam Bw.Badru Iddy amesema Banki tyake itaendelea kuwa karibu na wananchi kwani ni kawaida kwa Benki yao kutoa sehemu ya faida wanayoipata kwa wananchi ambao ndiyo wateja wao.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa Kituo cha Kigamboni Dr.Julius Nyakazilibe amesema kituo chake kinazidiwa na wagonjwa kutokana na ongezeko wagonjwa katika kata hiyo lakini pia kutokana na kata hiyo kuwa karibu na maeneo ya huduma kama shule,mahakama na kituo kikuu cha polisi cha Kigamboni.
Diwani wa kata ya Kigamboni Mh. Dotto Msawa ametoa shukrani kwa niaba ya wananchi wake amb apo ameipongeza Banki ya NMB hasa Meneja wa tawi la Kigamboni Bw.Nestory Mwombeki ambaye mara zote amekuwa tayari kusikiliza pale anapofika kuomba msaada kwa niaba ya wananchi.
‘’Huyu jamaa amekuwa rafiki yangu na ninapofika kwake amekuwa msaada kwetu wananchi wa Kigamboni, naomba msutuchoke’’ alisema Mh.Dotto Msawa.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa