Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni leo ameungana na wadau wa usafi kampuni ya Green waste na wafanyabiashara wa Kigamboni Feri kuhitimisha juma la Usafi kwa kusafisha mitaro na Barabara.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa usafi huo Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng’wilabuzu Ludigija amesema Halmashauri ya Manispaa imeona vyema kuhitimisha wiki ya mazingira na kuwakumbusha wananchi kufanaya usafi ili kujikinga ma magonjwa ya mlipuko yatokanayo na uchafu.
Ameongeza kuwa kampuni ya usafi ya Green waste ni wadau wa Kigamboni na kwamba viufaa vyao vya kisasa walivyonavyo vitasaidia kwa kiwango kikubwa kuweka Kigamboni safi lakini pia wananchi na wafanyabiashara wanao wajibu kuhakikisha maeneo yao ni masafi na wale wanaoishi kando ya barabara na mitaro hawatupi taka ovyo kwenye maeneo hayo.
“Wiki iliyopita tulifanya usafi kwenye mitaro yote ya Feri na kunyunyizia dawa ili kuua vimelea vya mbu vinavyosababisha ugonjwa wa dengue,Wananchi waone ni wajibu wao kuweka mazingira safi sio kusubiri hadi viongozi waje ndio waanze kuchukua hatua za usafi”Amesema Mkurugenzi
Aidha amesema amewaagiza watendaji wa Kata, Mitaa na Maafisa afya wote kuhakikisha wanasimamia suala la usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu kuhusu usafi wa kila mwisho wa mwezi na kwamba wale watakaoshindwa kutekeleza watalazimishwa.
Diwani wa Kata ya Kigamboni Mhe.Dotto Msawa amesema kuwa baada ya kuingia mkataba na kampuni ya usafi ya Green waste anatarajia kuwa Kigamboni inaenda kuwa ile aliyoitarajia na kuamini sasa itakua ya kwanza kwenye suala zima la usafi sababu kampuni hiyo inavifaa vya kisasa na wafanyakazi wa kutosha na kwamba hata changamoto ya ukusanyaji wa maji taka inaenda kutatuliwa sababu kampuni hiyo itasaidia kuleta magari yatakayokuwa yanavuta taka hizo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Green Waste Bw. Allan Sudi Amesema Manispaa imetoa mkataba wa kufanya usafi ambapo kwa kuanza wanaanza na Kata ya Kigamboni na baadae kusogea kwenye Kata 5 na kwamba wamejipanga kuhakikisha wanasambaza makasha ya kutosha ya kuhifadhia taka, kutoa eleimu kwa wananchi ya utunzaji mazingira na utupaji taka na kuchakata taka kabla ya kupeleka dampo ambapo eneo hilo la uchakataji wameomba Manispaa iwapatie.
Mkuu wa Idara ya Mazingira Manispaa ya Kigamboni Juvenalis Mauna amesema Manispaa itahakikisha kila mwananchi anafata taratibu za uhifadhi taka, kulipa tozo ikiwa ni pamoja na kutupa taka maeneo elekzi ili kuweka Mazingira safi kwa ustawi wa afya kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Manispaa mwenye suti ya kijivu Arch.Ng'wilabuzu Ludigija akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green waste wakipanga mikakati ya kuweka Kigamboni safi
Diwani wa Kata ya Kigamboni Mhe. Dotto Msawa mwenye kofia ya kijivuakishirikiana na wananchi wa Feri kufanya usafi
Mkurugenzi wa Manispaa Arch.Ng'wilabuzu Ludigija kushoto akisaidiana na Afisa Mazingira wa Manispaa Juvenalus mauna wakiweka uchafu kwenye gari la kukusanyia taka.
wafanyakazi wa green waste wakikusanya taka na kuziweka kwenye gari la kubebea taka hizo
usafi ukiendelea
wafanyakazi wa Manispaa na kampuni ya Green waste wakiendelea na usafi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa