Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Kigamboni Arch.Ng’wilabuzu Ludigija amewataka watumishi wa Hospitali ya Vijibweni na watumishi wote kwa ujumla kuepuka vitendo vya rushwa na kufanya kazi kwa bidii wakizingatia sheria taratibu na kanuni pamoja na ubunifu kazini.
Ameyazungumza hayo leo alipokuwa kwenye kikao cha watumishi wa h
Hospitali ya Vijibweni leo kkilichofanyika kwenye ukumbi wa Hospitali , Mkurugenzi amesema anataka kuona huduma za afya zinabadilika kwa kutolewa kwa upendo na ikiwezekana kuondoa ile dhana iliyopo kwa baadhi ya wananchi wanaoamini huduma bora za afya hazipatikani kwenye hospitali za Serikali.
Mkurugenzi amesema kuwa anajua watumishi wanaohudumu ni wachache lakini kwa uchache huohuo anawataka kufanya kazi kwa weredi kwa kuzingatia kanuni za utendaji kazi huku akisisitiza kuwa utumishi wa umma ni Utii kwa viongozi wanaowaongoza mbali na mapungufu ambayo wanaweza kuwanayo hao wanaowaongoza.
Aidha Mkurugenzi amewataka watumishi ambao wanafanya kazi kwa weredi kuwaripoti watumishi wanaowashawisishi kutokufanya kazi kwasababu ya masalahi ya posho na kwamba wakimbaini mtumishi wa namna hiyo wawe huru kumripoti kwa Mkurugenzi ili aweze kumchukulia hatua stahiki kwa kuleta ushawishi mbaya kwa watumishi.
Mkurugenzi amesema anatamani kuona Kigamboni inakuwa ya Mfano kwa utoaji mzuri wa huduma za afya kuanzia mapokezi mpaka mwisho wa huduma ili watu watoke maeneo mbalimbali kuja kujifunza namna kazi zinatekelezwa na sio uwepo wa majungu unaosababisha kushuka kwa ufanisi wa baadhi ya watendaji wazuri wa kazi unaosababishwa na watendaji wachache ambao hawajui thamani yao ya nafasi walizopatiwa.
“Natamani mama mjamzito anayekuja kuhudumiwa leba aone kama ni sehemu salama na nzuri kwake, vifo vitakavyojitokeza viwe kwa bahati mbaya lakini sio vya kusababishwa na mtumishi kwa utoaji mbaya wa huduma”Alisema Mkurugenzi.
Aidha Mkurugenzi amesisitiza kuwa upandishwaji wa vyeo kwa watumishi kwa sasa utazingatia utendaji kazi wa mtumishi ikiwa ni pamoja na uwajibikaji wake uliopo kwenye mpango kazi na kwamba ili akupandishe cheo ni lazima vyombo vya usalama vihusike ili kujiridhisha na mwenendo wako wa kikazi.
“kupanda vyeo sio kama zamani kwamba ukifika muda Fulani ni lazima upande, sasahivi ni lazima upimwe,na mimi napenda watumishi wawajibikaji na wanaojituma , mtumishi anayetekeleza wajibu wake kwa ukamilifu nipo tayari kumpigania kwa namna yoyote ile” alisema Mkurugenzi.
Wakati huohuo Mkurugenzi amemtaka Mganga Mkuu wa Wilaya kuwa ndio mtoaji wa ED (EXCEMPTION FROM DUTY) kutokana na uhuru mbaya wanaotumia watumishi kwa kutumia kigezo hicho na kwenda kufanya kazi kwenye hospitali binafsi hali na kusema kuwa huo ni uvivu na utumizi mbaya wa mishahara inayotolewa na Serikali bila kuifanyia kazi.
Mkurugenzi amewataka wajumbe wa menejimenti ya Hospitali (CHMT) kuwa washauri kwa Mkurugenzi na warekebishaji na sio kuondoa thamani ya utendaji kazi wa vituo na kuwataka watumishi wote,Makatibu wa Afya kufanya majukumu yao kwa weredi.
watumishi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi
watumishi wa afya wakimsikiliza Mkurugenzi kwa umakini
Baadhi ya watumishi
Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt CHarles Mkombachepa akipokea maagizo kutoka kwa Mkurugenzi na kuahidi kuyatendea kazi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa