Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale aipongeza timu ya mpira wa netiboli ya Manispaa ikiongozwa na kocha Mathew Kambona kwa kushika nafasi ya pili kwenye mashindano yaliyoshirikisha timu 16 za Manispaa za Dar es Salaam ,timu za jeshi pamoja na timu nyingine za Mitaani kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza Kitaifa yaliyofanyika Viwanja vya Manazi mmoja Dar.es Salaam kuanzia tarehe 7 -14/11 /2020.
Pongezi hizo amezitoa leo ofisini kwake alipokuwa akikabidhiwa kikombe cha ushindi wa nafasi ya pili na kikombe cha nidhamu ya timu ambapo amewahamasisha wachezaji kuendelea na mazoezi ili waweze kushiriki mashindano mengine makubwa zaidi ambapo pia ameiahidi timu kuhusu kukamilika kwa kiwanja cha mazoezi baada ya wiki mbili.
Aidha kwa kupitia afisa michezo wa Manispaa Adolphina Hamisi, Mkurugenzi amemtaka kuweka mazingira rafiki hususani yatakayoiwezesha timu kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kutafuta mechi za kirafiki ili kuijengea uwezo timu.
Timu ikiwa pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa Ndg. Erasto Kiwale wakifurahia ushindi wa vikombe walivyoshinda
Msemaji wa Timu Hanifa Kishoma akimvalisha Mkurugenzi wa Manispaa Ndg. Erasto Kiwale medani ya ushindi
msemaji wa timu Hanifa Kishoma akipeana mono wa pongezi na mkurugenzi baada ya kumvaisha medani ya ushindi
Kapteni wa Timu Bi. Zaituni akimkabidhi kombe la ushindi Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg. Erasto Kiwale
Kocha wa timu Bw. Mathew Kambona akiwa ameshikilia vikombe vya ushindi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa