Katika kuelekea kilele cha mwisho Wa matumizi ya mifuko ya plastiki JUNI 1 Mkurugenzi Wa Manispaa ya Kigamboni Leo amepokea makasha(dustbin) mawili kutoka kampuni ya usafi ya green waste ya kuhifadhia mifuko ya plastiki yatayowekwa kwenye Kituo cha daladala Feri.
Akizungumza wakati Wa mapokezi ya makasha hayo Mkurugenzi Wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng'wilabuzu Ludigija amesema katika kutekeleza agizo la Makamu Wa Rais Green waste imetoa mapipa hayo ambayo yatakuwa msaada mkubwa kwenye eneo la feri ambalo kuna wafanyabiashara wengi na mzunguko mkubwa wa watu.
" ili wote tukae kwenye Mazingira safi lazima kutekeleza kwa pamoja agizo kusitisha matumizi haya ya mifuko " alisema Mkurugenzi
Ameongeza kuwa Kigamboni kama Manispaa ingependa kuendesha zoezi hilo kwa Amani na asingependa kufikia hatua ya kufikishana kwenye faini hali ambayo haitapendeza.
Mkurugenzi amesema amepita kwenye mduka na soko la feri kuwakumbusha wafanyabiashara juu ya kutii agizo bila shuruti na kusema kuwa katika kata zote 9 na mitaa 67 watendaji na wenyeviti watakusanya mifuko itakayohifadhiwa kwenye stoo ya mbwa maji na baadae kupelekwa kwenye maeneo husika ikiwa ni pamoja na kutoa Elimu kwa wananchi .
Kwa upande wake meneja wa kampuni ya Green waste Bw. Allan Saudi amesema makasha (dustbin) waliyotoa ni mwanzo wa kuweka mazingira safi ya Kigamboni ambapo wameomba yatumike kwenye zoezi la ukusanyaji wa mifuko pekee na baadae wataleta mapipa mengine kwa kuhifadhia taka ngumu .
“Tunamshukuru mkurugenzi na wananchi wa Kigamboni kwa ktupokea vizuri haya makasha tuliyotoa leo nimwanzo tu, tunayo mengi sana tutayaleta hapa Kigamboni tulisha sikia miaka ya nyuma kido alipo kuja aliye kuwa Rais wa Marekani Barack Obama hadi bara bara zilipigwa deki tuanataka sasa hayo yafanyike hapa na kuanzia tarehe saba mtaona haya”Alisema Sud.
Aidha Afisa Mazingira wa Mnispaa ya Kigamboni Juvelus Mauna ,aliesema kupokelewa kwa makasha hayo nimoja ya hatua za kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani .
Boda boda wa kituo cha ferry wamesema hawatambeba abiria yeyote atakaye kuwa na mfuko wa Plastick kuanzia juni mosi mwaka huu.
makasha yaliyotolewa na kampuni ya kufanya usafi ya Green waste.
Ziara kueleeka kwenye maduka na soko la feri
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch. Ng'wilabuzu Ludigija akizungumza na baadhi ya wamiliki wa maduka kuhusu kutii agizo la matumizi ya mifuko mbadala.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Mhandisi. Ng'Wilabuzu Ludigija akimsisitiza jambo mwenyekiti wa soko la feri alipotembelea kukumbusha matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mwenyekiti wa Soko la Feri akimtoa hofu mkurugenzi juu ya utekelzaji wa agizo la Serikali
ukaguzi wa mitaro inayohifadhi mifuko ya plastiki inayopepea
Wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi ya Green waste wakikokota makasha kwaajili ya kupeleka mahali yatakayokuwa yamewekwa kwa kuwekea mifuko
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa