• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Care Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu ya awali na Msingi
      • Kilima mifugo na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondary
      • Mipango na uratibu
      • Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda biashara na Uwekezaji
      • Miundombinu ,Vijijini na Mjini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa jamii na Lishe
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
        • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa ndani
      • Usimamazi wa Manunuzi
      • Maliasili na uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na uhasibu
      • Usimamizi na usafi wa Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Utumishi
    • Huhuma za Kisheria
    • Usafi wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu
    • Michezo na Sanaa
  • Madiwani
    • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
      • Huduma za jamii
    • Ratiba za Vikao
      • Vikao vya Waheshimiwa
      • Kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
      • Miradi ya Sasa
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Picha
    • Hotuba
    • Gazeti la Mtandaoni
    • Vipeperushi
  • Mifumo

Miradi yenye thamani Bilion 3.4 yazinduliwa Kigamboni

Posted on: July 8th, 2018


Jumla ya miradi  saba yenye thamani ya shilingi bilioni 3.4  imezinduliwa, kuwekewa jiwe la msingi na kutembelewa katika Wilaya ya Kigamboni na mkimbiza Mwenge Mkuu wa Mwenge kitaifa mwaka 2018 ndg Charles Francis Kabeho.

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule mpya   ya sekondari katika kata ya Kigamboni unaojengwa kwa fedha za ndani ya halmashauri, mradi wa maabara ya kuzalishia vifaranga vya samaki ndani ya bustani ya wanyama ya Dar Es Salaam Zoo pamoja na mradi wa viwanja vya makazi, biashara na viwanda vidogo na vikubwa vilivyopimwa kwa ushirikiano kati ya manispaa ya Kigamboni na kampuni ya Property International.

Viwanja hivyo ni sehemu ya mpango kabambe wa mipango miji ya manispaa ya Kigamboni unaolenga kuboresha makazi ya wananchi kwa kupunguza ujenzi holela.

Miradi mingine ni uwekaji wa jiwe la msingi katika Chuo cha Afya cha Kigamboni City College of Health and Allied Sciences ambacho mpaka sasa kina jumla ya wanafunzi 726 wanaosoma kozi za utabibu, famasia na maabara katika ngazi za Astashahada na Shahada,mradi wa  kiwanda cha kukoboa na kusaga unga kilichopo kata ya Kimbiji ambacho kimeweza kutoa ajira kwa zaidi ya watu 60 ambapo mbali na kuwapongeza wawekezaji wa kiwanda hicho lakini pia aliwapa ushauri wa namna bora wanavyoweza kutafuta masoko ya ya bidhaa zao nje ya mkoa wa Dar es salaam na hata nje ya nchi kulingana na mahitaji

Mradi wa ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni pia uliwekewa jiwe la msingi na kiongozi mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 ambapo jengo hilo litakapokamilika litawapunguzia watumishi adha ya kukosa ofisi za kutosha na pia adha kwa wananchi wanaolazimika kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutokana na ofisi za Manispaa kutokuwa pamoja.

Miradi hiyo yenye sura ya ushirikiano kati sekta binafsi na serikali inakwenda sambamba na ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 unaosema 'Elimu ni Ufunguo wa Maisha ,wekeza sasa kwa maendeleo ya taifa letu ambapo msisitizo wa serikali ya awamu ya tano ni kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule ni lazima apelekwe shule kwani elimu kwa saa inatolewa bila malipo kuanzia elimu ya awali hadi sekondari.

Mwisho Kiongozi mkuu wa mbio za Mwenge wa Uhuru alikabidhi baiskeli maalum kwa kwa walemavu 26 kati ya 47 waliotarajiwa kukabidhiwa baiskeli hizo.


Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Hashim Mgandilwa akimpokea mkimbiza Mwenge wa uhuru Kitaifa Ndg.Charles Kabeho tayari kwa kuukimbiza Wilaya ya Kigamboni.

kikundi cha vijana wa hamasa wakisherehesha wakati wa mapokezi wa Mwenge wa Uhuru


Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya wakiwa tayarai kuupokea Mwenge wa Uhuru leo katika viwanja vya shule ya Msingi Ufukoni

Mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kigamboni

Kaimu Mkuu wa Idara ya Elimu ya Sekondari akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi shule ye sekondali Kigamboni.

Mmiliki wa Dar es salaam zoo akitoa maelezo namna anavyototolesha vifaranga vya samaki kwa mkimbiza Mwenge Kitaifa

moja ya bwawa lenye samaki wanaofugwa kisasa katika shamba la utotoleshaji  vifaranga vya samaki

Mkurugenzi Mtendaji wa Property Internation limited bw.Haleem  Zahran akionesha moja ya ramani ya viwanja walivyoviandaa.

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Charles Kabeho akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mkurugenzi Mtendaji wa Kigamboni Bw.Stephene Katemba  ishara ya kuonesha mradi wa viwanja umetembelewa

Mbio za mwenge wa Uhuru zikiendelea eneo la Kimbiji


Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa nDg.Charles Francis Kabeho akifungua kibao cha uzinduzi wa kiwanda cha kusaga na kukoboa mahindi kilichopo Kimbiji.

Viongozi na wananchi mbalimbali wakisikiliza ujumbe wa Mwenge eneo la Kimbiji.


ukaguzi wa kiwanda cha kusaga nak kukoboa mahindi ukiendelea kabla ya kuzinduliwa.


Mwenge wa Uhuru ukiwa umewasili eneo la mradi wa kiwanda cha kusaga na kukoboa mahindi


Jengo la chuo cha Afya Kigamboni uliowekwa jiwe la Msingi na Mwenge wa Uhuru 2018.


Mwenge wa Uhuru ukiwasili kwenye mradi wa uwekaji jiwe la Msingi wa Chuo cha afya kilichopo Kigamboni Mwembe mdogo.

Viongozi wakiongozwa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kibeho wakisoma maandishi ya kwenye jiwe la Msingi chuo cha Afya Kigamboni mara baada ya kuufungua.

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa akizungumza na klabu ya wapinga rushwa wa chuo cha afya Kigamboni.


wanachama wa klabu ya wapinga rushwa wakinyoosha vidole kujibu maswali ya Mkimbiza Mwenge Kitaifa Kabla ya uzinduzi wa Klabu hiyo.


Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.CHarles Kabeho akipanda mche wa mti ikiwa ni ishara ya kufungua klabu ya wapinga rushwa ya chuo cha afya Kigamboni.


Hatua ya ujenzi wa jengo la Utawala Manispaa ya kigamboni lililowekewa jiwe la msingi na Mwenge wa Uhuru 2018.

mwonekano wa ubavuni mwa jengo la utawala.


ramani ya jengo la utawala baada ya kukamilika


Ukiguzi wa jengo ukiendela.


Viti vya magurudumu vilivyotolewa na shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania kwa minajili ya kuwasaidia watu wenye ulemavu Manispaa ya Kigamboni.

mmoja wa wanaufaika wa baiskeli za magurudumu akisaidiwa kuketi kwenye baiskeli yake ikiwa ni ishara ya utoaji wa vifaa hivyo.

Mnufaika wa baiskeli ya magurudumu akishikana mkono na mkimbiza mwenge kitaifa ishara ya ugawaji wa baiskeli hizo kwa wawakilishi.


Watumishi na wakazi wa Kigamboni wakisikiliza risala ya utii

Katibu tawala wa Wilaya ya Kigamboni akisoma risala ya utii mbele ya halaiki kwenye viwanja vya Mji mwema kabla ya kuanza mkesha wa Mwenge wa Uhuru

Matangazo

  • Tangazo la Frem za Biashara, Soko la Kibada February 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye usaili nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi February 24, 2025
  • Tangazo la uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Afya March 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kazini nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi March 12, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIBADA - MWASONGA

    April 25, 2025
  • MANISPAA YA KIGAMBONI IMEPOKEA VITI MWENDO 35 NYENYE THAMANI YA TSH MIL 8

    April 08, 2025
  • MKANDARASI TOKA SUMA JKT ATAKIWA KUANZA MAPEMA MAANDALIZI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA TUNGI

    April 08, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele amefanya ziara ndani ya Manispaa ya Kigamboni

    March 22, 2025
  • Angalia Zote

Video

Makala maalumu ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Kigamboni
Video zingine

Kurasa za karibu

  • Municipal councilors
  • Kigamboni Municipal History
  • Investment Opportunities
  • Fomu ya Maombi ya Kiwanja
  • Huduma za Afya na Orodha ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni

    Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam

    Simu: +255222928468

    Simu ya Mkononi: +255222928468

    Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa