Hadi kufikia Desemba 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ilikua miongoni mwa Halmashauri zilizobahatika kupokea fedha kutoka Serikali kuu chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Kiasi cha milioni 400 ikiwa ni mpango wa maboresho ya vituo vya afya kote nchini.
Kituo cha Afya Kimbiji kilianza uboreshaji wake kuanzia Februari 2018 ambapo kililenga kujenga majengo ya mama na mtoto,chumba cha upasuaji,maabara ya kisasa, na jengo la kuhifadhia maiti ambalo hapo awali halikuwepo.
Hadi kukamilika na kuanza kutoa huduma kwa kituo hiki kiasi cha shilingi milioni 514.4 zimetumika ambapo Serikali kuu ilitoa kiasi cha shilingi milioni 400 na Manispaa kuchangia kiasi cha Milioni 114.4 ili kuboresha zaidi huduma za Afya kwa wakazi wa Kimbiji na maeneo ya Jirani.
Kituo hiki kimekamilika kwa asilimia 100 na huduma zote zinatolewa ambapo hadi kufikia Juni 2020 upasuaji 60 zimefanyika kwa ufanisi na mafanikio makubwa.
Aidha Watumishi wapatao 32 wa afya wenye fani mbalimbali wamepelekwa kwenye kituo hicho ili kuboresha utoaji wa huduma za afya zinazotolewa mahali hapo.
“Hadi kufikia juni jumla ya operation 60 zimefanyika, 25 za mama wajawazito na 35 nyingine, operation zote zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa”.
Muuguzi mfawidhi wa Kituo cha Afya Kimbiji Magdalena Msambazi alisema, idadi ya wagonjwa imeongezeka kutokana na kuboreshwa kwa kituo hicho cha afya kwani wamekuwa wakipokea wagonjwa wa rufaa wanaotoka kwenye zahanati za Pemba mnazi, Buyuni, Yaleyale puna na mwasonga.
Aidha alisema pia idadi ya wamama wanojifungua imeongezeka kutoka wazazi 15 waliokuwa wanazalisha kwa mwezi hadi kufikia wazazi 40 ambapo wazazi hao wamekuwa na amani ya kwamba ikishindikana kujifungua kawaida wanaweza kupata pia huduma ya upasuaji ambayo inatolewa kituoni hapo.
Muuguzi mfawidhi amemshukuru Rais wa awamu ya tano kwa kusaidia kuboresha huduma hizo za afya kwa wananchi wa Kimbiji na maeneo ya jirani kwani wananchi wanofika kupata huduma wanapata kwa wakati tofauti na awali ambapo kulikua hakuna.
Kituo cha Afya Kimbiji pia kinausafiri wa gari la wagonjwa linalosaidia kusafirishia wagonjwa kupelekwa nje ya kituo cha kimbiji( Hospitali ya Vijibweni) kwaajili ya kuhudumia wagonjwa pindi huduma iayopaswa kutolewa inaposhindikana kwa ngazi ya kituo hicho cha Afya.
Uboreshwaji wa kituo hiki cha Afya umewezesha wananchi wa Kimbiji na maeneo yote ya jirani kuepukana na adha ya kutembea umbali mrefu wa KM.75 waliokuwa wanaupata kwenda kufata huduma za afya mbali na makazi yao lakini pia umeondoa vifo vya mama na mtoto vilivyokuwa vinasababishwa na ukosefu wa huduma ya haraka.
Muonekano wa jengo la mama na mtoto
wodi ya wazazi.
jengo pacha la maabara na chumba cha upasuaji
ndani ya chumba cha upasuaji
maabra ya kisasa
muonekano wa ndani ya maabara
muonekano wa ndani ya maabara na vifaa vya kisasa vikiwepo kwaajili ya utendaji kazi
muonekano wa ndani ya maabara.
Jengo la kuhifadia maiti
Majengo ya kutolea huduma ya kimbiji yaliyokuwa yanatumika kabla ya ujenzi wa majengo mapya
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa