Ikiwa ni mwendelezo wa Serikali wa kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa kwa wananchi wote, Halmshauri ya Manispaa Kigamboni Julai 2018 ilipokea tena kiasi cha shilingi Milioni 400 kutoka Serikali kuu ili kuboresha kituo cha afya Kigamboni ambacho kabla ya upanuzi kilikua na changamoto ya kuzidiwa na wagonjwa hali iliyopelekea kudhoofu kwa utolewaji wa huduma.
Upanuzi wa kituo cha afya kigamboni umefanikisha kuongeza majengo ya mama na mtoto, jengo la kuhifadhia maiti ambalo halikuwepo hapo awali, jengo la upasuaji na maabara ya kisasa yenye vifaa vyote ambapo hadi sasa ujenzi umekamilika na huduma zote zimeanza kutolewa.
Mganga Mfawidhi wa kituo hiki cha Afya Kigamboni Dkt. Sophinias Ngonyani alisema kuwa, uboreshwaji wa kituo hicho kwanza kumewezesha kuboresha mazingira ya kazi, lakini pia kusogeza huduma kwa wananchi hususani huduma hii ya mama na mtoto.
Maganga aliongeza kusema kuwa awali kabla ya majengo hayo kujengwa walikuwa na chumba kimoja cha kuzalishia ambapo kwa wastani walikuwa wakizalisha wazazi 40-50 kwa mwezi lakini baada ya uboreshwaji wameweza kuzalisha wazazi 200 – 250 na jengo hilo linyeuwezo wa kuchua wazazi 8 ambao wanaweza kujifungua kwa wakati mmoja.
Huduma za upasuaji ambazo zilikuwa hazipatikani hapo awali zimeanza kutolewa tangu 1/12/2019 ambapo hadi kufikia june 2020 jumla ya wagonjwa 280 wameweza kufanyiwa upasuaji wa wazazi na magonjwa ya kinamama ambao kabla ya huduma hiyo iliwalazimu kupewa rufaa kwenda Temeke au Muhimbili.
Mganga mfawidhi ameshukuru Serikali kwa kuboresha huduma za Afya na kusema kuwa maabara ya kisasa yenye vifaa vyote imewezesha kutoa huduma nzuri na kwa wakati, na jengo la kuhifadhia maiti ambalo halikuwepo awali limewezesha wananchi kuhifadhi miili ya ndugu zao na kupata muda wa kujipanga namna bora ya kuweza kuendesha misiba pindi inapotokea.
Uboreshaji wa kituo hiki umewezesha wananchi kupata huduma zote bora na kwa wakati hususani kupunguza vifo vya mama na mtoto pamoja na kupunguza kuzidiwa kwa wagonjwa kulikokuwa kunasababishwa na ufinyu wa majengo ya kutolea huduma.
muonekano wa Maabara kwa ndani.
Maabara
Maabara
Vifaa vya Maabara
Vifaa vya maabara
Jengo la upasuaji
wodi ya wazazi
Chumba cha kuhifadhia maiti
Gari la wagonjwa la kituo cha Afya Kigamboni
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa