Halmashauriya Manispaa ya Kigamboni leo imetoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya vijanana watu wenye ulemavu kutoka kwenye asilimia 10 ya mapato yake ya ndani yenyethamani ya milioni 150 na vitambulisho vya wazee 600 kwaaajili ya huduma yamatibabu Bure.
Akizungumzawakati wa utoaji wa mikopo hiyo Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kiagmboni Mhe.Sara Msafiri amempongeza Mkurugenzi na Baraza la Madiwani kwa utekelezaji waagizo la Serikali na namna ambavyowamewezesha kuinua ukusanyaji wa mapato uliopelekea upatikanaji wa fedha hizoza Mikopo.
Aidhaameviasa vikundi 31 vinavyopokea mikopohiyo kutumia vyema na kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuinua uchumi badala yakufanyia mambo ambayo hayana tija na baadae kushindwa kurejesha Mikopo kwawakati ili wengine waweze kukopa.
Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiriamezindua awamu ya pili ya utoaji wavitambulisho vya matibabu kwa wazee ambapo jumla ya wazee 600 watapatiwavitambulisho hivyo kwenye ngazi ya kata.
Mkurugenziwa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng’wilabuzu Ludigija amesema kuwa kwa kipindi chamwaka wa fedha 2018/2019 Manispaailitenga asilimia kumi ya mapato yandani yenye thamani ya shilingi milioni 537.13 kwaajili ya utoaji wa Mikopo isiyo na Riba ambapo hadi sasa jumla yamilioni 400 zimekwisha tolewa kwa kipindi cha Julai 2018 hadi machi 2019.
Akizungumziautoaji wa Vitambulisho vya matibabu kwawazee Mkurugenzi amesema kuwa awamu ya pili vitambulisho 1000 vitatolewa kwawazee waliotambuliwa kwenye kata zotetisa ambapo kwenye uzinduzi huu jumla yavitambulisho 600 vinatolewa kwa wazee hao.
Manispaaya Kigamboni ina Jumla ya Wazee 4808 waliotambuliwa ambapo awamu ya kwanza ya utoaji wa vitambulisho vyamatibabu jumla ya wazee 2518 walipatiwa .
Mmoja wa wanakikundi akipokea hundi ya fedha kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri
Mkurugenzi wa Manipsaa ya Kigamboni Arch.Ng'wilabuzu Ludigija akizungumza na vijana na wazee walioshiriki kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri akizungumza na vijana waliofika kukabidhiwa hundi za mikopo na wazee waliofika kupokea vitambulisho vya matibabu.
baadhi ya vijana waliofika kupata hundi za mikopo
Mmoja wa wazee akipokea kitambulisho cha matibabu bure kwa furaha kwenye uzinduzi wa awamu ya pili utoaji wa vitambulisho kwa wazee.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa