Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Hashim Mgandilwa ameongoza zoezi la upandaji miti ya Mikoko katika fukwe za bahari ya hindi katika mtaa wa Pembacenter kata ya Pembamnazi.
Akiongea katika zoezi hilo jana , Mh.Mgandilwa amewapiga marufuku wananchi wa kata ya Pembamnazi kufanya shughuliza kibinadamu na kuwaasa kuwa walinzi wa mikoko hiyo kwani wao ndiyo wa kwanza watakao athirika kutokana na athari za uharibifu huo unaosababishwa na shughuli za binadamu .
alisema kuwa eneo ambao limepandwa miti lenye ukubwa wa zaidi ya hekari kumi limeharibiwa baada ya wananchi wa maeneo hayo na maeneo ya jirani kukata miti na kuchoma mkaa jambo ambalo ni hatari kwa mazingira.
"Mbali na kilimo, wakazi wa kata ya Pembamnazi mnategemea shughuli za uvuvi wa bahari kuendesha maisha yenu ya kila siku ambapo mikoko ni mojawapo ya mazalia ya samaki hivyo ni muhimu kuhakikisha miti hiyo inakuwepo kila wakatai bila kuharibiwa kwa namna yoyote"Alisema Mkuu wa Wilaya.
Kwa upande wa mratibu wa utunzaji wa mikoko kutoka TFS Ndg.Francis Kiondo amesema wao kama wakala wataendelea kutoa elimu kwa wananchi ambao ndiyo wanatakiwa kuwa walinzi .
Aidha aliongeza kuwa katika maeneo ambayo mikoko imekatwa wananchi wameanza kuathirika baaada maji ya bahari kuingia katika makazi na mashamba yao jambo ambalo lisipodhibitiwa linaweza kusababisha janga kubwa la kimazingira ikiwa ni pamoja na mazalia ya samaki kutoweka.
Zoezi hilo lililoratibiwa na Idara ya Mazingiza na misitu kwa kushirikiana na wakala wa misitu nchini TFS limewezesha upandaji wa miti elfu kumi katika siku ya kwanza huku lengo likiwa ni kupanda miche laki moja katika ukanda wonte wa bahari ya Hindi.
Mkuu wa Wiyala akiongea na wananchi waliofika katika zoezi la upandaji miti kabla ya zoezi kuanza
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa akiwa amebeba mfuko wenye miche ya Mikoko
Mkuu wa Wilaya Mh.Hashim Mgandilwa akipanda mche wa mkoo katika fukwe za bahari ya Hindi kata ya pembamnazi, pembeni ni viongozi na wananchi wakishiriki upandaji.
Katibu tawala wa Wilaya ya Kigamboni Bi.Rahel Mhando akipanda mche wa Mkoko
Maeneo ya fukwe yanavyoonekana baada ya wananchi wa maeneo hayo kukata miti kwa shughuli za kibinadamu.
Wanannchi wakisikiliza maelekezo ya namna ya upandaji miti
Wananchi wakisikiliza maelekezo ya namna ya upandaji miti
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa